Nafasi Ya Matangazo

October 14, 2022

Baada ya taarifa kutapakaa mitamdaoni ikimuonesha Mwanafunzi mhitimu wa Darasa la Sand katika Shule ya Msingi Chalinze Modern akilalamika kubadilishiwa namba ya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi uliofanyika mapema mwezi huu, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametoa kauli yake na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati Mamlaka husika zikilifanyia kazi suala hilo ukiwepo uchunguzi. 

Hii hapa Kauli ya Mbunge, Kikwete...
"KWANZA baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema niendelee kuwapongeza tena Wana -Chalinze kwa ushirikiano ambao kila siku umekuwa unaleta Mafanikio katika Mambo mbalimbali ndani ya Halmashauri Yetu.

Siku imekuwa na mazuri na Yanayofikirisha ndani yake.

Nimepokea taarifa zinazomuhusu Bint yetu anayeitwa Iptosum Suleiman Slim kuhusu shida iliyotokea kwenye Mitihani yake ya Darasa la Saba katika shule ya Msingi ya Chalinze Modern. Binafsi nieleze kwanza masikitiko kwa tukio zima maana linatupa nafasi ya kuhoji juu ya ukweli wa habari nzima. 

Si jema kwa Mwanafunzi, Shule wala Halmashauri yetu ya Chalinze. 

Asubuhi nimeuelekeza Uongozi wa Halmashauri yetu na Shule kutafuta jawabu ya changamoto hii. Nimewataka kuhakikisha jamii inapatiwa taarifa za ukweli kuhusu tukio zima na kama itakuwa kuna yeyote aliyehusika kuweka mazingira haya ikiwa ni dhuruma kwa mwanafunzi wetu huyu au kuchafua sura ya Shule yetu basi hatua za msingi kupata haki zifuate. 

Elimu ni kipaumbele chetu, kusomesha watoto wa kike ndiyo njia ya ukombozi wetu. Ninaamini Halmashauri yetu yenye wajibu wa kusimamia Elimu watatoa taarifa punde kama nilivyoelekeza.
 
Tunaomba Utulivu wakati jambo hili linafanyiwa kazi hili tupate muafaka wake. Ninaamini Haki itatendek kwa pande zote zinazohusika.

Niwatakie Kazi Njema"

Aidha tayari Baraza la Taifa la mitihani (NECTA) kupitia Afisa Habari na Mahusiano wake John Nchimbi imetoa taarifa ya kukufuatilia suala hilo na kuhakikisha mhusika anapata haki yake.




Posted by MROKI On Friday, October 14, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo