Nafasi Ya Matangazo

October 16, 2022

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhandisi Stella Manyanya akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Kamati katika mradi wa JNHPP. Kulia ni Mhandisi Lutengano Mwandambo mhandisi mzawa.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhandisi Stella Manyanya akimsikiliza Mhandisi Athanasius Nangali Kaimu mkurugenzi mtendaji -usambazaji (aliyesimama akizingumza) wakati wa kikao cha majumuisho  wakati wa ziara hiyo ya Kamati katika mradi wa JNHPP ambapo wakati wa majumuisho Manyanya alisema Kamati imeridhishwa na hatua za ujenzi kufikia asilimia 74 ikilinganishwa na asilimia 67 zilizopita na kulipongeza shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa kusimamia vema mradi huo na kumekuwepo na mabadiliko ya wazi yanayoonekana kila wakati.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika ziara ya kukaga mradi huo wa JNHPP.
Mhandisi Lutengano Mwandambo mhandisi mzawa wa mradi huo akifaanua jambo.
Na Neema Chalila Mbuja, JNHPP
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere unaotekelezwa na mkandarasi kutoka Misri wa kampuni ya ELSEWEDY na kugharimu kiasi cha shilingi  Trilioni 6.5 pindi utakapokamilika na hivyo kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme bora na uhakika kwenye gridi ya Taifa.
 
Akizungumza wakati wa majumuisho baada ya kutembelea mradi huo, kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa kamati imeridhishwa na hatua za ujenzi kufikia asilimia 74 ikilinganishwa na asilimia 67 zilizopita na kulipongeza shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa kusimamia vema mradi huo na kumekuwepo na mabadiliko ya wazi yanayoonekana kila wakati.
 
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Usambazaji Mhandisi Athanasius Nangali amesema kuwa kwa sasa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa mradi vimeshawasili ikiwemo TRANSFOMA 29 za njia moja zenye ukubwa wa 92.2 MVA ambazo zitatumika kwenye kituo cha kupoza umeme kutoka kampuni ya ABB.
 
Kamati ya Bunge ya kudumu ya Nishati na Madini ilitembelea eneo linakojengwa tuta kuu la kuhifadhi maji yaani main Dam ambalo lina sehemu kuu tatu yaani upande wa kushoto, kulia na kati na urefu wa mita 1025 na kimo cha mita 190 kutoka usawa wa bahari.
 
Eneo lingine walilotembelea ni jengo la mitambo yaani power house ambapo itasimikwa mitambo 9 yenye uwezo wa kufua umeme wa Megawati 235 kwa kila moja, pia walifanikiwa kuona hatua zinazoendelea eneo  zilikosimikwa mashine Umba yaani Transfoma ambazo zitatumika kwenye kituo cha kupooza umeme kabla ya kusafirishwa kuingia kwenye gridi.
Posted by MROKI On Sunday, October 16, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo