Nafasi Ya Matangazo

October 14, 2022

Mhandisi mkuu wa matengenezo Benjamin Mghuna akitoamaelezo juu ya mradi wa Kinyerezi II wakati kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea mradi huo wa kuchakata gesi asilia na mvuke.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. Dustan KItandula (Kulia) akimsikikiza Mhandisi Mkuu wa matengenezo Benjamin Mghuna alipokua akitoamaelezo juu ya mradi wa Kinyerezi II wakati kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea mradi huo wa kuchakata gesi asilia na mvuke.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. Dustan KItandula (Kulia) akiwa katika ziara hiyo na Kamati ya Bunge.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. Dustan KItandula akisistiza jambo.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiwa katika ziara katika mitambo ya TANESCO 
Moja ya eneo la mitambo ya kuzalisha umeme ya TANESCO.
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. Dustan KItandula akizingumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo.
*********

Na Neema Chalila Mbuja
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. Dustan KItandula amesifu jitihada zinazofanywa na TANESCO kuhakikisha mtambo wa kuchakata gesi wa Kinyerezi unazalisha kwa ufanisi na kwa kiwango Cha Hali ya juu

Mh. Kitandula ameyasema hayo wakati kamati ya Nishati na Madini ilipotembelea kituo hicho Cha kuchakata gesi asilia na mvuke Cha Kinyerezi II ambapo pamoja na Mambo mengine ameitaka Tanesco kuendelea kuangalia vyanzo vingine vya kuzalisha umeme pasipo kutegemea maji ili kuhakikisha huduma Zinaboreka kwa wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa huduma za usambazaji umeme Mhandisi Athanasius Nangali, ameahidi kuhakikisha miradi yote ya kimkakati inakuwa na tija ili kuboresha huduma.

Kituo Cha Kinyerezi kilianza ujenzi wake Machi 8, 2016 na kukamilika Machi 7 2019 ambapo ujenzi wa mradi umegharimu kiasi Cha Dola za kimarekani Milioni 344 sawa na fedha za kitanzania Bilioni648, na unazalisha Megawati 240.

Mpaka Sasa Kituo Cha kuchakata gesi Cha Kinyerezi II kina mitambo  8 inayotumia gesi asilia yaani Gas turbines ambapo Kati ya hiyo 6 unatimia gesi asilia pekee na 2 unatumia mvuke.

Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Nishati na Madini inatarajia pia kufanya ziara yake kwenye mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere jumamosi hii
Posted by MROKI On Friday, October 14, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo