Balozi
wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Dkt. Jilly Elibariki Maleko (aliyevaa miwani) akitembelea
mabanda ya wajasiriamali ya Watanzania alipotembelea mabanda hayo wakati wa Tamasha
la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea
nchini Burundi.
Balozi
wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Dkt. Jilly Elibariki Maleko (aliyevaa miwani) akitembelea
mabanda ya wajasiriamali ya Watanzania alipotembelea mabanda hayo wakati wa Tamasha
la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea
nchini Burundi.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Dkt. Jilly Elibariki Maleko (aliyevaa miwani) akitembelea mabanda ya wajasiriamali ya Watanzania alipotembelea mabanda hayo wakati wa Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea nchini Burundi.
Na Eleuteri Mangi, WUSM
Balozi wa Tanzania nchini
Burundi Mhe. Dkt. Jilly Elibariki Maleko amesema Watanzania wamehamasika na
wamekuja kwa wingi katika Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya
Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika kuanzia Septemba 4-12, 2022 nchini
Burundi.
Mhe. Balozi Dkt. Jilly amesema
hayo Septemba 06, 2022 mara baada ya kutembelea mabanda ya wajasiriamali kutoka
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walioleta bidha zao kwenye hilo.
Nimemaliza kutembelea mabanda
ya Tanzania na nchi nyingine, nimeona hamasha kubwa sana Watanzania waekuja kwa
wingi, watu mbalimbali wameleta bidhaa za Sanaa, chakula na kwa sababu Burundi
wanapenda sana bidhaa za chakula kutoka Tanzania. Nimeona jinsi
wanavyochangamkia mchele, dagaa, viungo vya chakula, mafuta, nguo batiki,
mapambo ya mwili na picha za Tingatinga, kwa kweli maonesho yamefana” amesema Mhe.
Balozi Dkt. Jilly.
Mhe. Balozi Dkt. Jilly
ameongeza kuwa ofisi yake inashirikiana pamoja na watanzania ambao wamekuja
kweny tamasha hilo kwa kuwahamasisha watu mbalimbali wakiwemo Wtanzania waishio
nchini Burundi, jamii ya kimataifa wakiwemo Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao,
wafanyakazi wa mashirika pamoja na kikanda na kuwahimiza kutembelea mabanda
yote ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Pamoja na maonesho hayo ya
Sanaa na Utamaduni, mada mbalimbali ziliwasilishwa tamasha hilo kiwemo jukumu
la teknolojia ya kisasa kwa kutumia utamaduni, tasnia ya sanaa na utalii, ushiriki
wa vijana katika shughuli za sanaa katika jumuiya ya EAC pamoja na matokeo ya
uvumbuzi katika sanaa na utamaduni.
0 comments:
Post a Comment