Muonekano wa baadhi ya majengo ya Kituo cha Afya cha Kata ya Ntuntu ambayo yanaendelea kujengwa.
Na Suzan Kajinga, Ikungi DC
HALMASHAURI ya Wilaya Ikungi mkoani Singida inaendelea kukamilisha miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwepo ya ujenzi wa vitu vya afya.
Moja ya ujenzi unaotekelezwa kwa kasi ni wa Kituo Cha Afya Kata ya Ntuntu
ambao umepiga hatua kubwa ambapo Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara na kichomea taka ujenzi wake
umefikia asilimia 80.
Majengo mengine yanayoendelea kujengwa ni Jengo la Mama na Mtoto ambalo
limefikia hatua ya nguzo mlalo (Linta)
na Jengo la kufulia ambalo lipo katika hatua
ya ukamilikaji huku Jengo la Upasuaji likiwa kwenye hatua ya upauaji.
Hatua hiyo nzuri ya ujenzi wa kitu hicho cha afya umefikiwa na usimamizi
mzuri wa ujenzi wa halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
hiyo Justice Kijazi, Mkuu wa Wilaya, Mbunge, Diwani, Wananchi pamoja na
Wataalam mbalimbali ikiwepo na Mkandarasi.
0 comments:
Post a Comment