Nafasi Ya Matangazo

September 02, 2022

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo Dkt,Sophia Kashenge na Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Duka la wakala wa mbegu ASA  Kilosa.

Na Lucas Raphael,Morogoro
Wakala Wa Mbegu za Kilimo”ASA” imeanza kutekeleza agizo la serikali la kuweka Miundombinu ya Umwagiliaji katika shamba la Mbegu la Msimba Kilosa Mkoani Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katika shamba la msimba wilayani kilosa  mkoani Morogoro, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo Dkt,Sophia Kashenge alisema Wakala umeanza na hatua za awali za kuchimba visima vya Maji vitakavyo tumika kufunga Mitambo ya Umwagiliaji katika Mashamba hayo.

Dkt Kashenge alisema hadi sasa shamba la Msimba kuna Visima vitatu virefu ambavyo vyote vina toa Maji hali ambayo inaonesha dalili njema ya kuwa na Maji mengi kwa msimu wote.

Alisema kwa shamba la Msimba ambqlo lina Zaidi ya Hekta 300 zitawekewa miundombinu ya Umwagiliaji katika Mwaka huu wa Fedha ambapo itasaidia kuongeza uzalishaji wa Mbegu kwa msimu mzima wa mwaka.

‘’ Uzalisha wa Mbegu ni kipaumbele chetu,tumepewa maagizo na wizara ya Kilimo ya kuhakikisha ndani ya muda mfupi mashamba yetu tuwe tume weka miundombinu ya umwagiliaji na hili tumekwisha lianza kwa hapa Msimba’’ Alisema Dkt.Kashenga.

Aidha Dkt Kashenge alisema mkakati wa wakala  nikuongeza Uzalishaji wa Mbegu za Alizeti kwa maelekezo ya Wizara ya Kilimo ambapo kwa sasa uzalishaji ni Zaidi ya Tani 1000 huku malengo yam waka ujao ni Tani 5000 za Alizeti katika Mashamba yote ya Mbegu.

Alisema mashamba yatakayo wekewa miundombinu ya Umwagiliaji kwa mwaka huu wa fedha ni Pamoja na Shamba la Msimba wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro,Shamba la Mwele Mkoani Tanga ,Shamba la Ngara Mtoni Mkoani  Arusha Pamoja na shamba la Kilimi Mkoani Tabora.

Alisema hayo ndio mashamba ya wakala yatakayoanza kuwekewa miundombinu ya umwagiliaji na baadae mashamba yote yatawekewa miundombinu hiyo ambapo ni takribani Hekta 10,000 zitawekewa umwagiliaji kwa maelekezo ya serikali.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi alipotembelea shamba hilo alisema wakala wa Mbegu umeanza kupiga hatua kubwa za uzalishaji  wa Mbegu hasa kwa kuanza mifumo ya Umwagiliaji.

Alisema Mapinduzi makubwa yanafanyika katika sekta ya kilimo hasa ya kuacha kutegemea Mvua badala yake kuwa na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji hali itakayo pelekea mashamba hayo ukabiliana na hali ya ukame Pamoja na mabadiliko ya tabia Nchi na kuweza kuzalisha mbegu bora.

Alisema Shamba hilo ni muhimu sana katika uzalishaji wa Mbegu za serikali kutokana na uhitaji wa mbegu Nchini.

Alisema Bunge la Jamuhuri ya Muungano limeongeza bajeti kubwa kwa wizra ya Kilimo hasa katika sekta ya Uzalishaji wa Mbegu za Kilimo na kuongeza kuwa shamba hilo limekuwa lizalisha mbegu nyingi za Alizeti ambazo hupelekwa kwa wananchi tayari kwa kilimo.

Hata hivyo Prof.Kabudi alimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu Dkt.Sophia Kashenge kwa kuendelea kufanya kazi vizuri na uwajibikaji katika sekta hiyo ya Uzalishaji wa Mbegu za Kilimo.

Prof.Kabudi alisema hatua ya kuanza kuweka miundombinu ya Umwagiliaji katika mashamba ya wakala Nchini yataongeza tija ya mbegu kwa wingi na kuifanya Nchi iweze kujitegema na hata  kuuza mbegu hizo kwa nchi za Jirani.

Aidha Mbuge huyo katika hafla hiyo alizindua duka la wakala la kuuza      Mbegu kwa wananchi ambapo hapo awali halikuwepo katika eneo hilo hali iliyowafanya wananchi hao kutafuta mbegu hizo kwa umbali mrefu.

Posted by MROKI On Friday, September 02, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo