Nafasi Ya Matangazo

July 28, 2022

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akiongea na wachezaji na viongozi wa Timu ya Taifa  inayoshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola inayoanza rasminjijini Birmingham, Uingereza, kesho Alhamisi Julai 28, 2022, akiwa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo Mhe. Said Yakub, Mbunge wa Singida mjini Mhe Mussa Sima na Kaimu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Neema Msitha.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akiongea na wachezaji na viongozi wa Timu ya Taifa  inayoshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola inayoanza rasminjijini Birmingham, Uingereza, kesho Alhamisi Julai 28, 2022, akiwa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo Mhe. Said Yakub, Mbunge wa Singida mjini Mhe Mussa Sima na Kaimu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Neema Msitha.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akiongea na mwanariadha wa Marathon Alphonce Felix Simbu ambaye ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa Timu ya Taifa  inayoshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola inayoanza rasmi kesho Alhamisi Julai 28, 2022 jijini Birmingham, akiwa na Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo Mhe. Said Yakub.
Mabondia Yusuph Changalawe (kulia), Kassim Mbunwike (wa pili toka kulia), mwanariadha Alphonce Felix Simbu, bondia Alex Isendi na mwanariadha Andrew Rhobi wakiwa kambini jijini Birmingham tayari kushiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola inayoanza rasmi kesho jijini Birmingham, Uingereza, kesho Alhamisi Julai 28, 2022, 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa Timu ya Taifa  inayoshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola inayoanza rasmi kesho jijini Birmingham, Uingereza, kesho Alhamisi Julai 28, 2022, akiwa  na Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo Mhe. Said Yakub, Mbunge wa Singida mjini Mhe Mussa Sima na Kaimu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Neema Msitha.
**********
Na John Mapepele, Birmingham
Waziriwa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa ameitembelea timu ya wachezaji wa Tanzania inayoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola  Birmingham nchini Uingereza na kuitaka kupambana kufa na kupona ili kurejea na medali.


Mhe.Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 27, 2022 kwenye kambi ya timu hiyo huku akisisitiza kuwa watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan wana matumaini makubwa na timu hiyo hivyo hawana budi kulinda heshima kubwa waliyopewa na taifa kwa ujumla.

“Nawaomba tangulizeni uzalendo ili tuweze kushinda, hii ni vita  tunahitaji kupambana bila kujali idadi yetu wala kitu chochote. Tutashinda.”Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Aidha, amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuinua  na kuendeleza michezo kwa kuwa michezo ni chanzo. Ha ajira na uchumi kwa taifa kwa kutambua hilo ndiyo maana kwa mara ya kwanza Serikali  imeamua kutoa fedha nyingi kwa wachezaji watakaopata medali za dhahabu dola za kimarekani 10,000, shaba 7500 na fedha 5000 bado zawadi za jumla” amesisitiza  Mhe. Mchengerwa.

Pia ametumia tukio hilo kutoa pongezi kwa timu ya wanaume na wanawake ya KABBADI kwa kufuzu kuingia kwenye mashindano ya kombe la Dunia yatakayofanyika Oktoba mwaka huu nchini India.

Mhe Mchengerwa ameongozana na Mhe. Musa Sima Mjumbe wa Kamati ya Bunge inayosimamia wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na ndugu Saidi Yakubu Naibu Katibu Mkuu.
Posted by MROKI On Thursday, July 28, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo