Nafasi Ya Matangazo

July 30, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Wema Emmanuel (wapili Kulia) akimpa mkono wa Shukrani Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya CRDB,Chabu Mishwaro baada ya Bemki hiyo kukabidhi madarasa mawili, ofisi ya walimu, madawati zaidi ya 100 na viti vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 40 kwa shule ya Sekondari ya Chitego Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Kulia no Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Eliamini Mark Maffa na kushoto ni Kamimukurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa, Fortunatus Mabula.
Jengo la 
madarasa mawili, ofisi ya walimu, vyenye thamani ya Shilingi Milioni 40 vilivyojengwa na Benki ya CRDB kupitia sera yake ya kusaidia Jamii (CSI Policy). 
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Wema Emmanuel (wapili Kushoto) na Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya CRDB,Chabu Mishwaro wakizindua jengo hilo la madarasa. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Chitego, Peter Kalunju na Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chitego, Eliamini Mark Maffa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Wema Emmanuel akikata utepe wa uzinduzi wa jengo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Wema Emmanuel akizingumza wakati wa makabidhiano ya jengo la madarasa mawili na ofisi ya walimu Shule yaSekondari Chitego.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya CRDB,Chabu Mishwaro akizingumza.
Watumishi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Diwani wa Kata ya Chitego,Peter Kalunju akizingumza na kuishukuru Benki ya CDRB kwa msaada huo wa vyumba vya madarasa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chitego, Eliamini Markc Maffa akizingumza na kueleza changamoto zingine zinazoikabili Shule hiyo ikiwapo maji na umeme.
Wanafunzi wa Sekondari ya Chitego Wilaya ya Kongwa wakifatilia matukio katika makabidhiano hayo.
Maafisa wa Benki ya CRDB 
Viongozi wakikagua vyumba vya madarasa.

************
Na Mwandishi wetu, Kongwa
BENKI ya CRDB imekabidhi madarasa mawili, ofisi ya walimu, madawati zaidi ya 100 na viti vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 40 kwa shule ya Sekondari ya Chitego Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Wema Emmanuel amesema mchango huo wa Benki ya CRDB ni muhimu katika kukuza elimu Wilayani Kongwa.

“Mchango huu uliotolewa na Benki ya CRDB ambao una lenga katika kukuza na kuboresha viwango vya elimu katika wilaya yetu ya Kongwa ni muhimu na wakipekee kwani ujenzi wa madara haya umesaidia kuanzishwa kwa shule hii mpya,”alisema Mkuu wa Wilaya  Remedius.

Alisema Kongwa inakabiliana na changamoto ya uhaba wa madarasa, pamoja na kuboresha miundombinu ya utoaji elimu, hivyo hatua ya Benki ya CRDB kusaidia kusaidia vyumba vya madara itaiwezesha kufikia lengo la kuwapa watoto haki ya msingi ya kupata elimu, kama ilivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Malengo ya Maendeleo Endelevu(SDG) 2030.

Remedius amesema Shule ya Sekondari Chitego ni shule mpya kwa maana ya matumizi kwani imeanza kutumika rasmi mwaka huu 2022. 

“Shule hii imefanikiwa kusajili wanafunzi 94 kwa idadi ikiwa ni kidato cha kwanza tu kwa mwaka huu, Shule hii ilianza kujengwa kupitia nguvu za wananchi waliojitoa kwa hali na mali ambapo walifanikiwa kujenga madarasa 4 ambayo bado hayajakamilika hadi leo yakiwa na hali yenye matumaini kwani yamesha ezekwa na Serikali iliweza kuongeza jitihada na kufanikiwa kujenga madarasa 3 na ofisi 1 kupitia mfuko wa UVIKO 19 hivyo kufanya jumla ya vyumba vya madarasa kuwa tisa,” alisema Remedius.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya CRDB, Chabu Mishwaro amesema  wao wanatambua kuwapo kwa changamoto kubwa katika uboreshaji wa elimu na miundombinu yake na serikali pekee haiwezi kuikabili bila wadau wengine kuchangia.

Chabu amesema Benki ya CRDB kupitia mpango wake wa kusaidia jamii, iliguswa na mahitaji ya Sekondari ya Chitego na kuamua kutoa mchango wao na anaamini msaada huo kwa kiasi kikubwa utasaidia kutatua kero ya miundombinu ya madarasa sambamba na kuboresha mazingira ya utoaji elimu katika Shule ya Sekondari Chitego na Halmashauri ya Wilaya Ya Kongwa kwa Kiujumla ukizingatia kua shule hiyo bado ni mpya.

Aidha aliwataka wanafunzi na jamii ya wana Chitego, kuwa makini na kuzingatia utunzaji  wa miundo mbinu ya elimu mashuleni hasa madarasa na kuwaasa wanafunzi kuwa na nidhamu. 

“Ni vyema kuviishi vitu hivi viwili ikiwa ni Umakini na nidhamu, ambavyo vitatoa mwanga zaidi katika maisha yenu na hata wadogo zenu waweze kutumia hapo baadae,”alisema Chabu.

Chabu, aliwataka wadau wote wa elimu waweze kuunga jitihada katika kuinua viwango vya elimu kwa kutoa michango yao ya hali na mali ikiwa ni kwa taasisi na  wananchi wakawaida ambao pia wanapaswa kuchangia maendeleo ya nchi.
Posted by MROKI On Saturday, July 30, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo