Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Arnold Mvamba akiongea na waandishi wa habari katika ofissi ya umoja ya vijana wa ccm mkoa wa Iringa kuhusu bajeti ambayo imetolewa na serikali ya mwaka 202/2023
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wakimsikiliza mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Arnold Mvamba alipokuwa anaijadili bajeti ya mwaka 2022/2023.
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
UMOJA
wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa wameipongeza bajeti ya
mwaka 2022/2023 ambayo imewagusa vijana kwa kiasi kikubwa na wananchi wote.
Akizungumza
na waandishi wa habari mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Arnold Mvamba alisema
kuwa bajeti imewagusa kwenye maslai ya wananchi hasa vijana katika maeneo
ambayo Serikali imeondoa ada kutoka shule ya msingi hadi kidato cha sita jambo
ambalo linamanufaa na vijana wengi.
Mvamba
alisema kuwa vijana wengi walikuwa wanakatisha ndoto zao kwa kukosa ada hasa
kidato cha tano na sita hivyo serikali kuondoa ada hiyo kutasaidia kuwa na
vijana wengi wasomi.
Alisema
kuwa kufuta ada kwa Wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutakuwa
kumewapunguzia adha ya wazazi kutafuta ada na sasa watajikita kwenye shughuli
za kimaendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Mvamba
aliongeza kwa kusema kuwa Serikali kwenye bajeti hiyo imeongeza zaidi ya kiasi
cha shilingi bilioni 8 kwa ajili ya kuwakopesha vijana kwenye vikundi ili
wakuze mitaji yao.
Alisema
kuwa kufanya hivyo kutasaidia vijana wengi kujiajiri kwa kufanya shughuli zao
binafsi ambazo watasaidia kuajiri vijana wengi na kuongeza soko la ajira kwa
vijana.
Mvamba
aliwataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na
serikali na kuacha tabia ya kulalamika pasipo na sababu muhimu.
Aidha
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Arnold Mvamba alisema kuwa anakasilishwa na
vitendo vya ukatili wa kijinsia unaoendelea mkoa wa Iringa na kuwataka vijana
wa Iringa kuacha mara moja tabia hiyo.
Alisema
kuwa vitendo vingi vya ukatili wa kijinsia vinafanywa na vijana na ndio maana
vijana wengi wamefungwa miaka mingi jela jambo ambalo sio jema kwa vizazi
vijavyo.
Mvamba
alisema kuwa vijana
wajikite kwenye kufanya kazi ili waepukana na vitendo vya ubaki na ulawiti.
Alisema
kuwa ana mpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga kwa kazi nzuri
anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.
Alimazia
kwa kuwaomba vijana wengi kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi wa chama ili kupata mamlaka ya kuiongoza chama cha
mapinduzi CCM kwenye eneo ambalo anaona anafaa.
0 comments:
Post a Comment