Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Misigiri kilichopo Kata ya Ulemo wilayani Iramba mkoani humo kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. |
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza na wananchi katika mnada wa Kitukutu ambapo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge alipata fursa ya kuzungumza nao na kupokea kero zao. |
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Pius Sangoma akizungumza kwenye ziara hiyo. |
Na Dotto Mwaibale,Singida
WAKURUGENZI wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Singida wametakiwa kuhudhuria ziara
zote za mkuu wa mkoa huo za kusikiliza
kero za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi
bila ya kuwatuma wawakilishi wao.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge leo Juni 28, 2022 baada
ya kupata taarifa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,Mhandisi
Michael Matomora hayupo kwenye mkutano wa hadhara wakati akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Misigiri kilichopo Kata ya Ulemo wilayani Iramba kwa ajili ya kusikiliza kero zao.
"Mkurugenzi yuko wapi, hawa wananchi wakitoa kero nani atazitatua,
namwelekeza RAS (Katibu Tawala wa Mkoa) RC (Mkuu wa Mkoa) ninapofanya ziara
wakurugenzi wawepo na kama kuna ruhsa nijulishwe nafasi yake itawakilishwa na
mtumishi mwingine," alisema na kuongeza.
"Hapa nina Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania ( TANROADS) ana kazi
nyingi sana, nina Meneja Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA),nina
watu wa maji Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wapo hapa ni
kwasababu tunataka kero zao wazisikilize moja kwa moja kutoka kwa wananchi,"
alisema.
Dk.Mahenge alisema yeye ni mwakilishi wa rais hivyo kero za wananchi rais
atazipata moja kwa moja kwasababu wananchi wana haki ya kumweleza kero zao.
Alisema kulikuwa na ulazima gani kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ua
Iramba kwenda kuhudhuria mkutano wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania
(TACAIDS) kwanini asingetuma mwakilishi kwenda huko ili yeye (DED) ashiriki
ziara.
"Marufuku DC (Mkuu wa Wilaya) na nipate maelezo kama hakukuwa na mtu
mwingine wa kwenda huko mpaka aende yeye tu, hata aliyemwita alipaswa anieleze
mimi Mkuu wa Mkoa kwamba tunajua una ziara lakini tunamwitaji DED tuone kama ni
yeye tu ndo anatakiwa aende maana halmashauri ni taasisi," alisema.
Akizungumzia kero ya maji iliyotokewa na wananchi aliigiza Wakala wa Maji Safi
na Usafi wa Mazingira (RUWASA) mkoani
hapa kwamba wiki ijayo wananchi wa kijiji cha Misigiri waanze kupata mara baada
ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha kufunga transifoma ili mota
za kusukumia maji zianze kufanya kazi.
Kuhusu elimu aliwapongeza wananchi wa Wilaya ya Iramba kwa kuchangia fedha
za chakula kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 76 na za sekondari 25
hatua ambayo imesaidia wilaya hiyo kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa
taifa wa darasa la Saba na kidato cha nne.
"Msingi wa mwanafunzi kufanya vizuri ni pale tu anapokuwa hana njaa
akiwa darasani, nawashukru wananchi wa Iramba kwa kuendelea kuchangia fedha za
chakula," alisema.
0 comments:
Post a Comment