Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo leo Aprili 5, 2022 Bungeni
jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa
Minza Simon Mjika, aliyetaka kujua mipango a Serikali ya kudhibiti na kutoa
fidia kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu.
“Wizara hufanya doria
za mara kwa mara kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu na pia vituo viwili
vya askari vitajengwa katika maeneo ya Busega na Meatu” Mhe. Masanja amesema.
Ameongeza kuwa ili
kukabiliana na changamoto hiyo Wizara itaajiri askari 600 ambapo kwa sasa
maombi ya vibali vya kuajiri yamewasilishwa kwenye mamlaka husika.
Aidha amesema Wizara hutoa mafunzo ya mbinu za kujilinda
na kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu ambapo Jumla ya Halmashauri
za wilaya 17 zimepatiwa mafunzo.
Pia, Wizara imetoa namba maalum za
simu kwenye kila kanda za kiutendaji ili kuwezesha wananchi kutoa taarifa za
matukio ya wanyamapori bila malipo.
Kuhusu kifuta jasho na kifuta machozi Serikali
imetoa jumla ya Shilingi 790,721,500 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa
wananchi 3,598 na kwa upande wa Mkoa wa Simiyu Wizara inafanya uhakiki wa
maombi yaliyoletwa ili waanze kulipwa.
Amesema lengo la
kifuta jasho/machozi ni kupunguza makali ya madhara ya wanyamapori kwa wananchi
na kuwezesha wananchi kuwa mtazamo chanya juu ya uhifadhi na siyo kulipa fidia.
Serikali inatambua kuwa siyo rahisi kufidia uhai wa binadamu bali inawafariji
waathika kutokana na madhara waliyoyapata.
Utekelezaji huo ni kwa mujibu wa Mkakati
wa Kitaifa wa Kusimamia Utatuzi wa Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori
wa mwaka 2020/2021 – 2024/2025.
0 comments:
Post a Comment