
March 31, 2022

March 30, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri, Wabunge na viongozi mbalimbali wa Kisekta nchini kuzungumza na wananchi kuhusu kero zinazowakabili.
Rais Samia aliongea hayo leo Machi 30, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma wakati akipokea Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Ripoti ya TAKUKURU.
Rais Samia alisema kwamba kumekuweko na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali sokoni hasa mafuta ya kula pamoja na mafuta ya petrol na diseli ambapo ni matokea ya mlipuko wa Ugonjwa wa COVID 19 duniani.
“Wabunge na Viongozi mnaosimamia Sekta waambieni wananchi ukweli waelewe yanayoendelea duniani, vita ya Russia na Ukraine imepandisha sana bei ya mafuta na kupelekea bei ya bidhaa zote kupanda kutokana na gharama za usafiri kupanda”, alisema Rais Samia
Aliongeza, mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 duniani pia umechochea mfumuko wa bei za bidhaa kwa kuwa bidhaa zote zilizohifadhiwa kwenye maghala zilitumika kwa vile uzalishaji ulisimama kwa kipindi chote ambacho hofu ya COVID 19 ilikuwa juu zaidi.
“Ukiangalia kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na kati, Tanzania ndio nchi yenye bei ya chini zaidi ya mafuta ambapo Serikali ilichukua hatua mbalimbali za kupunguza ikiwemo kuondoa tozo lakini bado bei iliendelea kupanda kwenye soko la dunia, viongozi waelezeni haya wanachi waelewe”, aliongeza Rais Samia.
Kuhusu suala la kupanda bei ya mafuta ya kula Rais Samia aliwaagiza viongozi wenye Sekta husika kuchukua hatua stahiki kwa suala hilo ili kuhakikisha wananchi hawakosi bidhaa hiyo sokoni.
“Nawaagiza viongozi waangalie suluhu ya changamoto ya mafuta ya kula, tulisimamisha kuingiza mafuta kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani, lakini hivi sasa viwanda vyote vya ndani vimesimamisha uzalishaji, nataka viongozi wangalie kama tunaweza kuyaruhusu sasa ili wananchi wasikose bidhaa sokoni”.
Kwa upande mwingine Rais Samia alitoa maelekezo kwa taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Bohari Kuu ya Madawa (MSD) kujichunguza na kujirekebisha ili kuhakikisha majukumu ya kila Sekta yanatekelezwa kwa wakati na kwa weliedi ambapo alisema viongozi wanaohusika na kutoa maamuzi wafanye hivyo bila kupoteza muda.
“Bohari Kuu ya Madawa naitaka ifanyiwe mabadiliko makubwa kuanzia ngazi ya uongozi wa juu mpaka kwenye vitengo vyake ili tuweze kwenda mbele, huko nyuma ilishafika hatua ya kupata tenda kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), lakini hatua iliyofikiwa sasa hata ndani watu wanalalamika hawapati huduma, kwa vile SADC bado wana imani nasi turekebishe ili twende mbele”, alisema Rais Samia.
Taasisi nyingine zilizoguswa na ripoti hiyo ni pamoja Mfuko wa Barabara Vijijini na Mjini (TARURA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Sekta ya Afya na Maji ambapo Rais Samia aliwataka wabunge kufanyia kazi hoja zote zilizowasilishwa kwenye ripoti hiyo kwa haraka na kutoa majibu kwa wananchi pindi watakapoenda bungeni.
March 27, 2022









March 21, 2022
Sheha wa Kojani, Hamad Ali Bakari akizungumza wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri waliozuru kisiwa cha Kojani hivi karibuni |
Kojani ni kisiwa cha wavuvi. Hatufanyi shughuli nyingine hapa. Ni uvuvi miaka nenda, miaka rudi. Maisha yetu ni samaki, watoto wanasoma shule na tunajitibu kwa mapato ya samaki. Tunasubiri kuona wataleta nini.
Nasikia kuna vyombo vitakuja. Tutaweza kwenda kwenye bahari kubwa. Tunasubiri, wakati wao ukifika tutaambiwa. Tukipata yote hayo kama ambavyo wanasema, patakuwa na mabadiliko makubwa ya maisha ya hapa.
Hapa kama mlivyoona maisha ni pesa. Ukitaka embe, kama ambazo mmekula kule ng’ambo, ni pesa. Kojani hakuna mashamba, kila kitu kinaletwa, utakila kama una pesa. Kama serikali itatufanya tuondokane na uvuvi huu mdogo itakuwa imetusaidia sana”.
Nukuu hizi ni za Sheha wa Kojani, Hamad Ali Bakari. Kisiwa cha Kojani, kiko pembeni mwa kisiwa kikubwa cha Pemba. Kina Shehia mbili, Kojani anakoongoza Bakari na Mpambani kwa Sheha Omary Ali Omary.
Bakari alikuwa akijibu swali kama amepata kusikia/anaujua mpango mkubwa wa Uchumi wa Buluu, wa Rais Dk. Hussein Mwinyi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, unaolenga kubadili maisha ya Wazanzibar kwa kuifanya Bahari na mazingira yake kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya nchi.
Ni wavuvi kama hawa wa Kojani walioenea katika maeneo mbalimbali ya nchi ambao Dk. Mwinyi na timu yake wamedhamiria kuwafikia na kubadili maisha yao.
Serikali ya Dk. Mwinyi imetenga shilingi bilioni 36.5 zitakazotumika kuwezesha makundi mbalimbali ndani ya jamii kushiriki katika mpango mzima wa Uchumi wa Buluu.
Na kwa wavuvi kama Sheha huyu, yaani wale wavuvi wadogowadogo wapatao 5,770, watapatiwa maboti yapatayo 577 na nyenzo mbalimbali za uvuvi ili kuwawezesha badala ya kuvua kilo chache tu za samaki kama walivyozowea, wakipata vyombo sasa waende kwenye kina kikubwa zaidi cha bahari na wavue samaki kwa tani na tani.
Anasema Dk. Mwinyi kwamba wamekusudia kuitumia Bahari kujenga Uchumi wa Buluu ulio endelevu kuwafanya wavuvi na makundi mengine kama ya Wanawake kushiriki katikia kujiletea maendeleo.
“Badala ya mvuvi kupata kilo mbili kwa sababu hawezi kufika kwenye kina kirefu, sasa awezeshwe kwanza kwenda kwenye kina kirefu cha bahari na awe na nyavu stahiki za kuvua samaki.
Tunasema shughuli hii iwe endelevu kwa maana kwamba ule uvuvi wa nyavu zisizostahiki au wa kupiga mabomu unaoharibu mazingira unaachwa," anasema Dk. Mwinyi.
Katibu Mkuu, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Dk. Aboud Jumbe |
“Unaleta faida za kijamii na kiuchumi kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo kwa kuchangia katika upatikanaji wa chakula, kuondoa umasikini, kuongeza ajira, kuimarisha afya, kuleta usawa na utulivu wa kisiasa, ” anasema Dk. Jumbe kwenye sehemu ya mada yake ya Uchumi wa Buluu aliyowasilisha katika Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri, mwezi huu, Zanzibar.
Dk. Jumbe anasema kwa ujumla kwa Zanzibar Uchumi wa Buluu utakuwa ni shirikishi ukilenga kupata ushiriki wa kila mmoja.
Ziara ya kisiwani Kojani imeisha, Wahariri wanarudi Chakechake, Pemba. |
WATANZANIA wametakiwa kuzingatia afya ya kinywa na meno kwa kuwa ndio ufunguo wa kuwa na siha njema.
Kauli hiyo imetolewa na mtaalamu wa masuala ya afya ya kinywa na meno, Dk Donna Williams- Ngirwa (pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Afya ya Kinywa na Meno.
Alisema ipo haja ya watanzania kuhakikisha kwamba wanashughulika na afya ya kinywa na meno kwa kuwa ndio mlango wa uhai na afya bora katika maisha yao.
Alisema katika mahojiano leo kuwa mtu akizimbea kushughulikia afya ya kinywa anakaribisha maradhi mbalimbali yakiwemo yaliyo sugu.
Dk Donna wa Afya Bora Complete Dentistry Ltd alisema kwamba maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbiu ya kimataifa ya ‘jivunia kinywa chako’ yana maana kubwa kwa kuwa kuzuia maradhi ya kinywa kwa kumtembelea daktari wa meno angalau mara mbili kwa mwaka husaidia sana.
“Magonjwa mengi ya kinywa na meno hayajitambulishi mpaka yamefikia hatua mbaya hivyo ni vyema kuwahi kuyagundua, ili uwe na siha njema” alisema.
Hata hivyo alitaja kuwepo na kampeni kubwa ya afya ya kinywa ili kujiweka sawa kama ufanyaji wa mazoezi unavyotumika kuweka sawa mwili.
“Kuna haja ya kuanzisha kampeni ya kuelimisha umma umuhimu wa afya ya kinywa kwa kuwa ndio mlango wa afya,” alisema na kuongeza kwamba ni watu waone umuhimu wa kujua wanachokula na madhara yake kwani ndio msingi wa afya njema ya meno na kinywa.
Anasema watu hawafikirii kuhusu uhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya yao kwa ujumla, kwani kinywa ndio ukuta wa kuzuia maradhi katika mwili.
Anasema maradhi ya kinywa yanapokuwa katika hatua za mwanzo ni rahisi kutibika lakini yanapokuwa katika hatua kubwa yanakuwa changamoto.
"Mtu anapokuwa na tatizo la kinywani huongeza hatari , kwa mfano ugonjwa wa rheumatoid arologist, atherosulinosis, shinikizo la damu, ugonjwa wa Alzheimers, ugonjwa wa sukari, na matatizo wakati wa kujifungua."
Alisema watu wanaougua matatizo ya kinywani , huwa na sababu tofauti zinazoweza kusababisha magonjwa mengine.
Kwa mfano, idadi kuu ya molekuli zinazozalishwa na seli za binadamu na kusababisha uvimbe katika ufizi zinaweza kufikia viungo vingine vya mwili na kusababisha athari katika maeneo hayo. Kumtembelea daktari wa meno ili kutibu matatizo hayo ya kinywa ni muhimu.
Dk Donna amesema kwa sasa wataalamu wa afya ya kinywa wamekuwa na vifaa vya kisasa zaidi hivyo ni rahisi kubaini matatizo kabla hayajawa sugu.
“Kwa mfano ninapofanya shughuli zangu tunafuata misingi ya kimataifa ya utoaji huduma kutokana na umuhimu wake,” alisema na kuongeza kuwa sekta hiyo ina teknolojia mpya.
Dk Donna ambaye pia alishiriki kuanzisha kliniki ya afya ya kinywa ya Morningside Dental Care, ya New York, Marekani mwaka 1995, alisema njia nzuri ya kuwezesha afya ya kinywa na meno ni kuhakikisha kwamba unamuona daktari wa meno ili aweze kukusaidia.
March 17, 2022
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana amewataka waraibu wa dawa za kulevya kutumia fursa za kliniki za kuponya zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini ili waweze kurejea katika hali ya kawaida kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Dkt. Zavery Benela alieleza kwamba , Kliniki ya MAT, Mwananyamala inahudumia wateja zaidi ya 1,350 kila siku ambao wanafika kupata huduma.
March 16, 2022
Waziri Dkt. Pindi alitoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau wa chaneli hiyo na Manaibu Mawaziri kwa lengo la kujadili mikakati na maboresho ya channeli ili kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwake.
Alisema kwamba baada ya uzinduzi wa Chaneli hiyo uliofanywa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Disemba , 2015 iliundwa kamati ya watendaji wa wizara kujadili na kutoa mapendekezo yatakayoboresha uendeshaji wake kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kimataifa.
“Moja ya mapendekezo ilikuwa ni kuhakikisha inapatikana katika visimbuzi vyote na majukwaa mengine nchini na hapa kuna wataalamu mtatuambia hii haitoshi tuweke na kwenye simu, mitandao ya kijamii ndiyo maana kikao cha leo kina wabobezi hivyo ni lazima tufikiri nje ya boksi kama tunazungumzia utalii siyo lazima mtu afike nyumbani ndipo awashe luninga yake zionekane hata katika vyombo vya usafiri,”alisema Mhe. Pindi.
Kuhusu athahari ya UVIKO -19 katika sekta ya utalii Mhe. Pindi alisema pato linalotokana na utalii lilishuka kutoka dola za Kimarekani Bilioni 2.532 mwaka 2019 hadi Bilioni 1.107 mwaka 2021 lakini bado inatajwa kama sekta muhimu kwa uchumi wa Nchi.
Hata hivyo Waziri Pindi alibainisha kwamba chaneli hiyo inapaswa kuwa endelevu na vipindi vinavyoandaliwa viwe vyenye ushawishi kwa wananchi kuvutiwa kutembelea vivutio vilivyopo nchini hata mataifa ya nje kutembelea vivutio hivyo.
“Vivile kikao hiki kitoe mapendekezo ya namna ya kupata fedha za dharula kwa jili ya kushughulikia uandaaji wa vipindi vipya na kuweka mikakati ya kuhakikisha uendelevu wa chaneli hii na kamati ya Mheshimwa Waziri Mkuu ilikutana Disemba 27, 2018 kuweka mikakati ya uendelevu wa chaneli ikiwemo ubora unaozingatia viwango vya kimataifa, uhitaji wa mafunzo, upatikanaji wa vifaa vya kisasa na kuwezesha chaneli kupatikana katika majukwaa yote,”alisisitiza Mhe. Pindi.
Alihitimisha kwa kusema masuala ya utalii ni mtambuka yanayoshirikisha sekta mbalimbali kama sekta ya utalii, sekta ya uchukuzi, sekta ya habari na mawasiliano na sekta ya fedha hivyo kama wasimamizi wa sera katika Wizara husika ipo haja ya kuifahamu chaneli hiyo, lengo la kuanzishwa na umuhimu wake kwa sekta ya utaliii na uchumi kwa Nchi.
Aidha Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji (TBC) Dkt. Ayoub Ryoba akaeleza mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa chaneli hiyo ambayo ni ununuzi na ufungaji wa mitambo ya kidigitali, kurusha matangazo kote Duniani, kurushwa vipindi vyake kupitia visimbuzi vyote nchini, kuboresha vifaa, kutoa elimu ya utalii kwa watanzania kuptia vivutio vya kiutamaduni, hifadhi za wanyama na utalii wa Ikolojia.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokuwa wakikagua Jengo la kuhifadhia Kumbukumbu za Mahakama lililopo Mahakama Kuu Tanga.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Ole Gabriel akionyesha moja ya maboksi maalum yanayotumika kuhifadhia majalada mbalimbali yanayohifadhiwa katika jengo hilo.
Mhe. Mwakasaka sambamba na Wabunge wenzake wa Kamati hiyo, leo wameaanza ziara ya kukagua Miradi ya Mahakama ambapo wameanza rasmi kwa kukagua Jengo jipya la kuhifadhi Kumbukumbu za Mahakama lililopo Mahakama Kuu-Kanda ya Tanga.
Mhe. Mwakasaka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maadili, Madaraka na Haki za Bunge alikiri wazi kuridhishwa na muonekano wa jengo hilo baada ya kulikagua na Wanakamati wenzake na kusema kuwa jengo ni zuri na litasaidia katika kuhifadhi vizuri kumbukumbu za Mahakama katika Kanda hiyo.
“Leo tumekuja kutembelea jengo hili ya kuhifadhi kumbukumbu, kwakweli jengo hili kwa kiasi kikubwa linaridhisha ukiachia mbali mambo madogo madogo ambayo Viongozi wameahidi watayafanyia kazi. Na nikiri wazi kuwa Mahakama mnaendelea vizuri,” aliongeza Mbunge huyo.
Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geofrey Pinda ameeleza kuwa wajibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ni kupitia/kukagua Miradi iliyopo chini ya mwamvuli wa Wizara hiyo ambamo ndani yake imo pia Mahakama ya Tanzania inayotekeleza Miradi mingi.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda, alisema hadi kufikia 2025 Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kusogeza huduma za miundombinu ya majengo huku akieleza kuwa Wilaya zote zitakuwa na Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo kwa kila Tarafa.
“Tunao uhaba mkubwa wa majengo ya Mahakama, ukiangalia katika ngazi ya Mahakama za Mwanzo, kati ya Kata karibia 3800 ni Kata 960 pekee zenye Mahakama za Mwanzo, hivyo lengo lililopo ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 kila Wilaya iwe na Mahakama na kwa upande wa Mahakama za Mwanzo angalau kila makao makuu ya Tarafa kuwe na Mahakama,” alieleza Mhe. Pinda.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel ameishukuru Kamati hiyo kwa ushirikiano na vilevile kuishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa rasilimali fedha zinazowezesha kuendesha miradi na shughuli mbalimbali za kimahakama akiongeza kuwa Mahakama ipo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga na kuwezesha mkoa huo kuwa na Mahakama za Wilaya kwa wilaya zake zote.
“Kwa niaba ya Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania napenda kutoa shukrani zangu kwenu ninyi Wahe. Wabunge kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mhimili huu unaotuwezesha kusonga mbele, vilevile pokeeni shukrani hizi kutoka kwa Mhe. Jaji Mkuu ambaye anatambua ziara hii ambayo mmeianza leo na ninaomba kuwahakikishia kuwa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkinga utakamilika mwisho mwa mwezi Aprili mwaka huu,” alisema Prof. Ole Gabriel.
Jengo hilo la kisasa la Kuhifadhi kumbukumbu za Mahakama lililokaguliwa limegharimu kiasi cha fedha za Kitanzania 139, 411,376/= na imeelezwa kuwa litasaidia kuongeza ufanisi katika kazi kwa kuokoa muda mrefu wa kutafuta majalada ambayo awali hayakuwa katika mpangilio mzuri, vilevile litasaidia kuleta uwazi na kuimarisha usalama wa kumbukumbu hizo muhimu.
Kamati hiyo inatarajia kufanya ukaguzi pia kwenye Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wavulana katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) -Lushoto, Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Same, Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mwanga na Ukarabati wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi-Kilimanjaro na mwisho Mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC)-Arusha.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo Cha Diplomasia Jijini Dar es Salaam |
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Stella Ikupa akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo Cha Diplomasia Jijini Dar es Salaam |