Nafasi Ya Matangazo

February 02, 2022

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mika Likapakapa ,akihutubia wananchi na Wana CCM katika sherehe za kuadhimisha miaka 45 tang kianzishwe chama hicho Februari 5, 1977 zilizofanyika kiwilaya Kata ya Iglanson.
Mkuu wa wila hiyo Jerry Muro akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Stamili Dendego akizungumza kwenye hafla hiyo

Katibu Mwenezi wa CCM  wa wilaya hiyo, Pius Sanka akiongoza sherehe hizo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mika Likapakapa akishiriki kupanda mche wa miti katika eneo la la kituo cha afya cha Kata ya Iglanson ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe hiyo.
Katibu Mwenezi wa CCM  wa wilaya hiyo, Pius Sanka  akipanda mche wa mti.
Kada wa CCM wa Wilaya ya Ikungi kutoka Kata ya Iglanson Joseph Ngerera Mwinamila (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro wakati wa sherehe hiyo walipo mtembelea nyumbani kwake. Katika ni Mwenyekiti wa CCM  Mika Likapakapa.
*********
Na Dotto Mwaibale, Singida
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa amesema wilayo hiyo Ikungi inajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama hicho Februari 5, 1977.

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 45 tangu kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kiwilaya Kata ya Iglanson jana alisema baadhi ya mafanikio wanayojivunia ni miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na serikali kwa gharama kubwa si kwa Ikungi tu bali kwa nchi nzima ambapo alimtaka kila kiongozi katika wilaya hiyo kuyatangaza mafanikio hayo ya Serikali ya kwanza hadi ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ili wananchi wayajue kwa kuiletea maendeleo wilaya hiyo kupitia  miradi ya mbalimbali.

Alisema kila kiongozi ana wajibu wa kuisaidia Serikali kuyatangaza mafanikio hayo wananchi wayajue kwani bila ya kufanya hivyo wanaweza wakaibuka wajanza na kuanza kueleza ya na kupotosha ukweli wa kazi kubwa iliyofanywa na serikali.

Alitaja baadhi ya miradi waliyoipata ni ya  ujenzi wa vituo vya afya na zahanati, maji, shule na miundombinu ya barabara.

Alisema katika wilaya hiyo wana vituo vya afya Kata za Irisya, Ntuntu, Iglanson ambavyo vipo hatua ya ujenzi wa Sh. 500 Milioni huku Kituo cha afya cha Sepuka na Ihanja vikiwa vimekamilika na hiyo yote ni kutokana na usimamizi mzuri ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM.

Likapakapa alitumia nafasi hiyo kuwataka wenyeviti wa vijiji kila mwaka kuitisha mikutano na kuwasomea mapato na matumizi ya fedha kama sheria inavyoelekeza na si vinginevyo.

Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro alisema moja ya jambo kubwa wanalojivunia sisi Serikali katika kipindi cha miaka 45 tulioyafanya na kumshukuru Mungu ni kusimamia usalama wa wananchi,mali zao na amani ya nchi yetu.

"Nataka kuwahakikishia kuwa kumlinda raia na mali zake watu waamke asubuhi waende mashambani, makazini, warudi nyumbani wapitie sehemu kupata kiburudisho na kurudi nyumbani salama sio jambo dogo kwani vijana wa usalama wanakuwa nje wakati wote kuwalinda.

Alisema mpaka tunafikia miaka 45 katika wilaya hiyo hakuna matukio yoyote makubwa ya kihalifu yaliyotokea ya uvamizi wa silaha, unyang'anyi na mauaji makubwa ya halaiki na wizi ni jambo la kujivunia sana na kuwa na Taifa lenye amani sio kazi ndogo kwani kuna mambo makubwa yanafanywa na vyombo vya usalama kuhakikisha nchi inakuwa salama na utulivu.

Muro alisema katika kipindi hiki cha miaka 45 wameshuhudi CCM ikikiisimamia Serikali na kuielekeza katika miradi yote mikubwa ya maendeleo na kuwa katika kipindi hiki cha miaka 45 mingine Serikali itahimalisha mtandao wake na kuhakikisha amani inaendelea kuwepo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga alisema katika kipindi hiki cha miaka 45 wanajivunia kuona Serikali ikitoa fedha nyingi za miradi mbalimbali katika wilaya hiyo na kueleza katika Shule Shikizi ya Isingisha walipata Sh.80 Milioni,Mwaru Sh.80 Milioni, Kizugi Sh.80 Milioni, Mnyange Sh.Milioni 40,Sekondari Sh.40 Milioni, Maji Iglanson Sh. 217 Milioni, Kituo cha Afya Kata ya Iglanson Sh.250 Milioni, Shule ya Msingi Iglanson Sh.53 Milioni, Maabara ya sekondari Sh.30 Milioni alisema fedha hizo karibu zaidi ya  bilioni 1 zimetolewa na Serikali katika kata moja tu. 

Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi Stamili Dendego akimkaribisha mgeni rasmi wa sherehe hiyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kufika kwa wingi na kueleza kuwa sherehe hizo katika wilaya hiyo zilianza Januari 24 na kuwa jumuiya ya vijana waliadhimisha sherehe hizo katika Kata ya Ntuntu, na Jumuiya ya Wazazi walihitimisha Kata ya Mkiwa huku UWT huku UWT wakihitimisha Kata ya Ikungi na kuwa leo Januari 2 kilele cha maadhimisho hayo kiwilaya yatafanyika katika Kata ya Mang'onyi.

Dendego alisema katika maadhimisho hayo kazi zilizofanyika ni kufanya usafi, kupanda miti kuzungunga Kituo cha Afya kinacho jengwa katika kata hiyo na kuingiza wanachama sambamba na kusajili watu kwa mfumo wa kielektoniki. 

Posted by MROKI On Wednesday, February 02, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo