Nafasi Ya Matangazo

January 25, 2022

Mjumbe  wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Asina Omar (kushoto) akiteta jambo na Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC Lesotho),  Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana akizungumza jambo
Wakiwa katika chumba cha kutangazia matokeo.
Mjumbe  wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Asina Omar (kulia) akiteta jambo na Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC Lesotho),  Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana akizungumza jambo
Mjumbe  wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Asina Omar akizungumza katika kikao hicha pamoja na ugerni kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC Lesotho), Kushoto ni Mjumbe wa IEC Lesotho, Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana akizungumza jambo
Mjumbe  wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Asina Omar akizungumza katika kikao hicha pamoja na ugerni kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC Lesotho).
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akizungumza katika kikao hicha pamoja na ugeni kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC Lesotho).
Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho,Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana akizungumza jambo.
Afisa Rasilimali watu,  Thato Moeti  akizungumza
Meneja Msaidizi wa Fedha Azael Limpho Monese
Wakurugenzi wa Idara wakiwa katika kikao cha pamoja na wageni wao


UJUMBE wa watu wa tatu kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEF Lesotho) ukuingozwa na Mjumbe wa Tume hiyo,Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana wapo nchini kwa ziara ya kimafunzo ambapo leo Januari 19,2022 wametembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma. 

Katika Ziara hiyo waliyoifanya katika Makao Makuu ya NEC, ujumbe huo ulipokelewa na Kaimu Mwenyekiti wa Tume, ambaye pia ni Mjumbe  wa Tume, Asina Omar na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Wilson Mahera Charles na kisha kuwatembeza katika jengo hilo na kujionea  shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi Tanzania.

Mjumbe huyo kutoka Tume ya Lesotho,  IEF Lesotho Dkt Monlakoana ameambatana na Maofisa kutoka Tume hiyo,  Afisa Rasilimali watu,  Thato Moeti  na Meneja Msaidizi wa Fedha Azael Limpho Monese.

Aidha ujumbe huo ulipata fursa ya kuzungumza na menejimenti ya Tume na baadae Mkurugenzi, Dkt Mahera akatoa wasilisho kuhusiana na Muundo,  majukumu na Kazi za Tume.
Posted by MROKI On Tuesday, January 25, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo