Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.
Joyce Ndalichako (Mb) akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu (hawapo pichani)
walioshiriki uzinduzi wa mradi wa Jifunze Uelewe uliofanyika mkoani Morogoro
katika shule ya msingi Chifu Albert Luthuli.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (Mb) akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa mradi wa Jifunze Uelewe uliofanyika mkoani Morogoro katika shule ya msingi Chifu Albert Luthuli.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiwagawia watoto wasioona kifaa maalum cha kusomea kwa wanafunzi wasioona (braille reader) vinavyotolewa na shirika la USAID wakati wa uzinduzi wa mradi wa Jifunze Uelewe uliofanyika mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkaazi wa shirika la USAID, Kate Somvongsiri akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa mradi wa Jifunze Uelewe uliofanyika mkoani Morogoro katika shule ya msingi Chifu Albert Luthuli.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akisoma moja ya vitabu vinavyotolewa na shirika la USAID wakati wa uzinduzi wa mradi wa Jifunze Uelewe uliofanyika mkoani Morogoro.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro, Germana Mung'aho akizungumza na wadau mbalimbali wa elimu (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa mradi wa Jifunze Uelewe uliofanyika mkoani Morogoro katika shule ya msingi Chifu Albert Luthuli.
**********
Na WyEST,
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amezindua mradi wa Jifunze Uelewe wenye
lengo la kuboresha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi wa awali hadi darasa la nne katika mikoa ya
Iringa, Morogoro, Mtwara na Ruvuma wakiwemo wenye mahitaji maalum.
Uzinduzi wa mradi huo
unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) umefanyika katika shule ya Albert
Luthuli mkoani Morogoro ikiwa ni kuunga
mkono jitihada za Serikali katika kuboresha utoaji elimu nchini kwa kuhakikisha
mazingira salama na jumuishi katika kusoma kwa watoto .
Amesema mradi huo utatoa
mafunzo endelevu kwa walimu kazini 25,578 katika shule 2,825 na kwamba
utanufaisha jumla ya wanafunzi 1,259,227 kutoka katika mikoa hiyo.
Aidha, Mhe. Ndalichako ametoa rai kwa wadau wote wa elimu kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote nchini wakiwemo wenye mahitaji maalum.
Niwaombe wadau wote wa elimu,
mashirika yasiyo ya kiserikali, makampuni binafsi na vyombo vya habari
kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha ushiriki wa pamoja ili
kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bora wakiwemo watoto wenye mahitaji
maalum," amesema Prof. Ndalichako.
Amesema mradi utatoa nyenzo za
elimu jumuishi ikiwemo vifaa kwa wasioona kama _braille readers_ za
kielektroniki, vitabu vya kielektroniki na vifaa vya lugha za alama.
Naye Germana Mung'aho ambaye
ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa
Mkoa huyo, ameishukuru Serikali na Shirika la USAID kwa kuona umuhimu wa kuinua
elimu mkoani humo na kuahidi kushirikiana bega kwa bega katika kutekeleza mradi
huu ili kufikia malengo yaliyowekwa.












0 comments:
Post a Comment