Nafasi Ya Matangazo

November 18, 2021

Ili kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji yako Mambo makubwa matano kama tutayasimamia basi kunaweza kuwa na migogoro michache au tukaimaliza yote. 

Akizungumza katika mkutano ulioitwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ndg. Aboubakar Kunenge, Mbunge wa Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete ameeleza kuwa Mambo ya Msingi ya kusimamiwa ni pamoja na Sheria zinazoongoza Shughuli za nchi, kutotembeza Mifugo na kuchunga maeneo yote, kutengeneza ranchi ndogondogo, Kuchimbwa mabwawa maeneo yenye mifugo mingi, na kuongeza umakini kwa wasimamizi wa sheria kwa uchache wake. 

Mkoa wa Pwani ni mmoja kati ya Mikoa iliyoathiriwa sana na migogoro ya Wakulima na Wafugaji ambapo watu wengi wameuwawa, kupata ulemavu na kupoteza mazao yao kwa sababu ya mifugo.
Posted by MROKI On Thursday, November 18, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo