Mwandishi wetu,Babati
Timu nane zimetinga hatua ya robo fainali katika michuano ya chemchem Cup ya kupiga vita ujangili katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya Wanyamapori ya jamii(JUHIBU)Wilayani Babati Mkoa wa Manyara.
Mratibu wa michuano hiyo,Walter Pallangyo amezitaja timu hizo kuwa ni Mdori Fc,Majengo ,Kisangani Fc na Macedonia FC.
Pallango alisema timu nyingine ni Manyara FC,Sangaiwe,Kakoi na Samta FC.
"Nusu fainali ya michuano hii itaanza Octoba 7 mwaka huu na Fainali itakuwa Octobea 11 katika viwanja vya mdori"alisema
Katika michuano hii ambayo hufanyika kila mwaka zaidi ya sh 70 milioni zinatumika ambazo zimetolewa na Taasisi ya Chemchem iliyowekeza katika hifadhi hiyo hoteli za kitalii na utalii wa picha.
Katibu wa michuano hiyo,Beno Alfred amesema timu 20 kutoka vijiji 10 vinavyounda jumuiya hiyo zilikuwa zinashiriki michuano hiyo.
Alfred amesema sambamba na soka pia kutakuwa na michuano ya mpira wa pete na timu ambazo zinashiriki ni Mwada,Walimu,Ngolei na Mdori.
0 comments:
Post a Comment