Nafasi Ya Matangazo

September 29, 2019

Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri,alipowasili kwa ajili ya kufungua mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri,akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Mifugo(LITA) Mpwapwa, Moses Mlahagwa anayefatia ni Afisa mifugo Mkuu Idara ya malisho na Rasilimali ya vyakula vya mifugo Israel Kilonzo alipowasili kwa ajili ya kufungua mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri,akisaini kitabu mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa kufungua Kikao cha mafunzo rejea kwa wataalam wa malisho kutoka mashamba ya Serikali na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika leo kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa na upande wa kulia ni Mkuu wa Kampasi Lita Mpwapwa yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkurugenzi wa Utafiti ,Mafunzo na Ugani kutoka wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo rejea kwa wataalam wa malisho kutoka mashamba ya Serikali na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Meneja wa shamba la kuzalisha malisho na mbegu za malisho Vikuge Kibaha Ricahard Mdegipala,akitoa taarifa katika kikao cha mafunzo rejea kwa wataalam wa malisho kutoka mashamba ya Serikali na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Sehemu ya washiriki kutoka sehemu mbalimbali wakifatilia ufunguzi wa mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Afisa Mifugo na Mtaalam wa malisho kutoka Mabuki Bi.Asteria Mwaya,akitoa taarifa wakati semina ya mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Mifugo(LITA) Mpwapwa, Moses Mlahagwa,akisisitiza jambo kwa wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Meneja wa Shamba la malisho Langwira Mbarali mkoani Mbeya ,akitoa taarifa wakati semina ya mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkurugenzi wa Utafiti,mafunzo na Ugani kutoka wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri mara baada ya semina ya mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Ugani kutoka wizara ya Mifugo Dkt.Mwillawa akitoa maada katika kikao cha mafunzo ya rejea kwa wataalam wa malisho kutoka mashamba ya Serikali na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Sehemu ya wataalam kutoka sehemu mbalimbali wakiendelea kuchangia mada katika semina ya mafunzo ya wataalam na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
*********************
Na.Mwaandishi wetu,Mpwapwa
Wataalamu wa malisho kutoka halmashauri mbalimbali hapa nchini, wametakiwa kutoa elimu hiyo kwa wafugaji ili kuwajengea uwezo wa kutambua matumizi bora na endelevu ya nyanda za malisho.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri wakati akifungua mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.

Mkuu wa Wilaya Shekimwer alisema elimu ya utunzaji malisho ni muhimu kwa wafugaji kwa sababu itawasaidia kujua nini wanatakiwa kufanya ili kudhibiti uhaba wa malisho pale unapotokea.

Alisema lengo lao ni kuona maafisa ugani hao wanatumia nafasi walionayo kutoa elimu hiyo kiufanisi kwa wafugaji katika halmashauri mbalimbali wanazotoka ambayo itasaidia kupunguza migogoro baina ya wafugaji na wakulima kugombea maeneo ya malisho.

"Mafunzo mliyoyapata mkayatoe kwa wafugaji katika sehemu mnazotoka tumieni nafasi yenu ili kuisaidia serikali ya awamu ya tano kuboresha sekta ya Mifugo," amesema Shekimwer.

"Mnapaswa kuhamasisha na kuongeza uvunaji wa malisho na matumizi ya teknolojia rahisi za kukata,kufunga,na kuhifadhi majani na masalia ya mazao ili yatumike wakati wa uhaba" alisema

Alisema kuwa hayo yakitekelezwa anaimani itasaidia wafugaji kujenga Utamaduni wa kusindika masalia ya nafaka na kuchakata kwa ajili ya kulisha Mifugo yao.

Pia ameiopongeza wizara ya Mifugo kutokana na kuwa mstari wa mbele kutoa mafunzo kwa maafisa ugani mara kwa mara ambayo yanasaidia kuwakumbusha majukumu yao ya kazi.

Aidha alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inalenga kuboresha sekta hivyo,hivyo ni vema maafisa ugani na wataalamu wa malisho kuzingatia elimu wanayopewa ili nao wakaitoe kwa wafugaji.

Awali akieleza lengo la semina hiyo, Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani Wizara hiyo,Dkt.Angello Mwillawa, alisema ili kukabiliana na changamoto pamoja na migogoro inayowakumba wakulima na wafugaji, wizara umeona iwakutanishe wataalam wa malisho nchi nzima ili kila mmoja aainishe changamoto anazokutana nazo katika eneo lake.

Dkt.Mwillawa aliwataka wataalam hao kuwa wa wazi kueleza changamoto zilizopo ili wizara iweze kufahamu wapi pa kuanzia katika kutatua changamoto na migogoro hiyo.

Akizungumzia changamoto ya upatikanaji wa mbegu za malisho ambayo ilielezwa na washiriki, alisema hakuna changamoto kama hiyo mbegu zipo nyingi tatizo ni uzembe wa wataalam hao katika kuagiza na kufuatilia kwa karibu ili ziwafikie katika vituo vyao.

Mkurugenzi huyo aliwataka kuhakikisha wanakuwa 'na mtandao bora na kubadilishana uzoefu baina ya eneo moja na jingine jambo ambalo litawapa wepesi katika kutatua kila changamoto.

Pia aliwataka kuongeza thamani katika bidhaa zao 'na kuainisha aina ya mbegu wanazozalisha na kuuza kwa wafugaji pamoja na faida au hasara yake hiyo itakuwa rahisi kufanya biashara.

Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo waliishukuru wizara kwa kuandaa warsha hiyo huku wakieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo uwezo mdogo wa kuendeleza maeneo yao hivyo kujikuta maeneo mengi yakubali kuwa vichaka licha ya kuwa na uhitaji wa maeneo.

Akizungumza Meneja wa Shamba la Malisho Vikuge wilayani kibaha mkoani Pwani, Richard Mdegipala, alisema wao wana eneo la ukubwa wa hekta 515 lakini hekta 215 ya shamba au eneo hilo ni pori wameshindwa kuliendeleza wakiiomba serikali iwasaidie.

Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Mifugo(LITA) Mpwapwa, Moses Mlahagwa, aliwataka wataalam hao kuhakikisha wanatafuta alama ya kuiweka watakaporejea katika vituo vyao vya kazi mara baada ya warsha hiyo ili kuonyesha kuwa ilikuwa na tija kubwa wao.

"Hapo mlipo mtambue kuwa mmebeba dhamana ya mifugo ya Taifa nanyi ndio mnaotarajiwa kubadili changamoto za wafugaji kuwa fulsa, jambo la muhimu kwenu mnalotakiwa kulifanyia kazi ni alama gani mnakwenda ukiacha,"alisema.
Posted by MROKI On Sunday, September 29, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo