Nafasi Ya Matangazo

September 30, 2019

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amekuwa ni kiongozi wa kuigwa katika taifa hili kutokanana na jinsi alivyosimamia maendeleo makubwa katika jimbo lake.
 Moja ya miradi aliyoitekeleza 
 Mikutano ya Chama


 Ujenzi wa miundombinu ya maji safi ni moja ya vitu alivyotekeleza.
Na Shushu Joel, chalinze.
JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania katika wilaya ya Bagamoyo,mkoani Pwani wamempongeza mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete kwa Utendaji wake wa kazi katika jimbo hilo.

Kwa kawaida wakulima walio wengi hapa nchini utumia muda mwingi katika shughuli ya kilimo kwenye kipindi cha masika lakini Mbunge wa Chalinze amekuwa akilima masika na kiangazi.

Maneno hayo yametolewa na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ,Rukia Masenga alipokuwa katika sherehe za maadhimisho ya Umoja huo ambayo kiwilaya yalifanyika katika Kijiji Cha Msoga, halmashauri ya chalinze.

Mbunge wa Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete amekuwa ni kiongozi wa kuigwa katika taifa hili kutokanana na jinsi alivyosimamia maendeleo makubwa katika jimbo lake.

"Sie Kama jumuiya ya wanawake tumeridhisha na utekelezaji wa ilani katika Jimbo lake"Alisema 

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amewashukuru kina mama hao kwa kuona kile kilichokuwa kinahitajika kwa wananchi kinatekelezeka kwa kiwango kikubwa.

Aliongeza kuwa chalinze imetekeleza ilani ya CCM kwa vitendo kutokana na kupunguza na kumaliza yale yaliyokuwa ni changamoto kubwa kwa Wananchi wa Halmashauri hiyo ikiwemo shida kuwa ya Maji na Afya ya Wakina Mama na Watoto.

Akizungumzia ujenzi wa Vituo cha afya katika Halmashauri ya Chalinze,Mh.MBunge alisema kazi kubwa imefanyika kujenga Zahanati kila kijiji na leo ni vijiji Vichache ambavyo Zahanati zao hazijakamilika. Kwa Upande wa Vituo vya Afya hali ni nzuri sana kila Kata ila kituo kasoro kata 3 ambazo nazo ziko mbioni kwenye Ujenzi. Kwa Upande wa Elimu wamejenga Vyumba zaidi ya madarasa 48,Umeme umesambazaa katika jimbo zima la Chalinze na Miundombinu ya Barabara inakwenda vizuri na Serikali imepanga kutumia 158.5 Milioni kwa ajili ya Barabara za Mji wa Chalinze ambazo zitajengwa kwa kiwango cha Rami na madaraja madogo.

Katika Jambo jengine Mh.Mbunge Kikwete ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuipatia Chalinze Shilingi Bilioni 16 kwa ajili ya kutatua changamoto ya Maji iliyokuwa ni changamoto kubwa sana miaka ya nyuma. Fedha ambazo amezieleza kuwa zinakwenda kumaliza shida ya maji sio tu kwa wana chalinze lakini kwa Maeneo ya miji ya Jirani hasa Ngerengere, na Magindu kwa upande wa Kibaha Vijijini.

Mh.Mbunge pia amewapongeza wanawake kwa jinsi wananvyokuwa mstali wa mbele katika ufanisi wao wa kuchangamkia fursa ndondogo za halmashauri. Hadi sasa vikundi zaidi ya 80 vya wanawake vimeweza kufikiwa katima kqta mbalimbali lakini kubwa pia ni jinsi wanavyorudisha mikopo hivyo. Kwa hakika nyie ni wa kipekee,mh. Mbunge alimaliza.

Ziara ya Mheshimiwa Mbunge inaendelea.
Posted by MROKI On Monday, September 30, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo