Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Serikali imetangaza kiama kwa
wanaochelewesha mbolea kuwafikia wakulima kwa wakati kwani kuchelewa kwa mbolea
ni miongoni mwa sababu zinazopunguza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya wakulima
nchini.
Mbolea kutofika kwa wakulima
kwa wakati ni wazi kuwa Taasisi iliyopewa jukumu la kusimamia na kudhibiti
mbolea ya TFRA imeshindwa kufanya kazi yake kwa ufasaha hivyo ikibainika
kuchelewa kwa mbolea pasina sababu za msingi watendaji hao watachukuliwa hatua
za kisheria.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) ametoa kauli hiyo ya onyo leo tarehe 4 Julai 2019 Jijini Dar es
salaam wakati akizungumza kwenye kikao kazi na wafanyakazi wa Taasisi ya udhibiti
wa mbolea Tanzania (TFRA).
Alisema kuwa mbolea
inayohitajika kwa wakulima ni Lazima ipatikane kwa wakati katika maeneo ya
kilimo. “Kupatikana kwa wakati maana yake ni kwamba kila mtu anapoishi anapaswa
kuipata kirahisi kupitia maduka au masoko” Alisema
Aliongeza kuwa kazi ya
Taasisi ya udhibiti wa mbolea Tanzania ni kuhakikisha mbolea inawafikia
wakulima sio kusalia Jijini Dar es salaam ilihali wakulima wapo mikoa yote
Tanzania na endapo mbolea ikikosekana kwa wakulima watendaji wa TFRA
watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kadhalika alisema kuwa
kupatikana pekee kwa mbolea kwa wakulima ni jambo moja lakini muhimu ni kuwa na
bei nafuu ambazo wakulima wataweza kuzimudu.
“Sasa hivi kuna malalamiko
mengi kwa wakulima kuwa mbolea zinauzwa bei ya juu hivyo wameshindwa kuzimudu, haiwezekani
mbolea itoke Ulaya ikiwa na bei nafuu lakini kumfikia mkulima inakuwa na bei
ghali, hapo ni wazi kuwa TFRA hamjafanya kazi yenu sawasawa” Alikaririwa Mhe
Hasunga
Alisema kuwa endapo TFRA
itatekeleza majukumu yake ipasavyo mbolea itapungua bei na wakulima watanufaika
na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais
wa Tanzania.
“Na kama tatizo la gharama
linaongezeka kutokana na usafirishaji kuna sababu gani za kutumia magari
kusafirisha wakati kuna usafiri muhimu wa reli (TRC) ambapo mawakala wangepakua
na kusambaza mizigo hiyo baada ya kufika katika maeneo mbalimbali inapoishia
reli” Alisema
Hata hivyo amesisitiza kuwa
serikali imeanzisha mchakato wa kupitia mbolea kote nchini ili uagizaji wa
mbolea iweze kuagizwa itakayoendana na uwezo wa udongo.
0 comments:
Post a Comment