Nafasi Ya Matangazo

April 11, 2019

Mwandishi wetu.Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla (pichani) anatarajia kutua wilayani Longido, hivi karibuni, kutatua mgogoro baina ya  Kampuni ya  Uwindaji ya Green Miles Safari Ltd  inayomiliki kitalu cha Lake Natron wilayani Longido na vijiji  23 vinavyozunguka kitalu hicho.

Vijiji hivyo, vinaidai kampuni hiyo,  kiasi cha sh 329 milioni kutokana na makubaliano ambayo wamefikiwa ambapo licha ya suala hilo kufikishwa ngazi ya halmashauri, wilaya na mkoa kampuni hiyo inadaiwa kumegoma kulipa.

Akizungumza jiji hapa, Waziri Kigwangalla alisema, baada ya kupokea ujumbe wa viongozi wa wilaya ya Longido kutaka wizara hiyo kutatua mgogoro huo, wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Frank Mwaisumbe, Mkurugenzi a halmashauri, Jumaa Mhina na madiwani, atakwenda Longido.

"Nitakwenda Longido kutoa maamuzi ya serikali  baada ya kuzisikiliza pande zote"alisema Kigwangalla

Kampuni ya Green Miles ambayo tayari imesitishiwa huduma na Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori(TAWA)  kutokana na kushindwa kutimiza kanuni za umiliki wa vitalu,imekuwa na mgogoro na wananchi wa vijiji vya Longido na serikali mkoani Arusha.

Naibu Kamishna wa Utalii na Biashara wa TAWA, Imani Nkuwi alisema kampuni hiyo, imeshindwa kulipa ada za kutotumia zaidi ya asilimia 40 ya mgao wa kuwinda katika vitalu.

"kampuni hii tumeinyia huduma za kuwinda katika vitalu vyake vyote  wakati suala lao likifanyiwa kazi"alisema.

Kampuni hiyo, inamiliki vitalu wilayani Longido na katika pori la akiba la Selous  na katika siku za karibuni, imekuwa na migogoro na vijiji ilipowekeza wilayani Longido.

Hivi karibuni,  Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe alitoa agizo , kukamatwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Green Miles  Salim Abdalah Awadhi, kutokana na kushindwa kulipa madeni ya vijiji na halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha.

Mwaisumbe alisema vijiji 23 vya wilaya hiyo, vinaidai kampuni hiyo, kiasi cha sh 329 milioni kutokana na makubaliano walioingia tangu mwaka 2017/18.

Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Longido, Wakili Jumaa Mhina, alisema ofisini yake imekuwa ikiitaka  kampuni hiyo  kulipa fedha za vijiji na halmashauri bila ya mafanikio.

"mimi nimekuwa nikimtaka aje kulipa ni dawa ya migogoro kwani ndugu zangu hawa masai ni watu waelewa lakini imeshindikana"alisema

Hata hivyo,Mkurugenzi wa Green Miles Safari Ltd, Salim Abdalah Awadhi  amekuwa akikanusha tuhuma mbali mbali dhidi ya kampuni yake,ikiwepo kudaiwa na vijiji fedha. 

Wakati Mgogoro huo wa madai ukiendelea, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameunda kamati ya vyombo vya ulinzi na usalama na uhifadhi, kuchunguza kwa kina chanzo cha kuuawa na Majangili Twiga 25 wilayani Longido na 16 kati yao katika kitalu cha kampuni hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka watendaji wa kampuni hiyo, kujitokeza kutoa maelezo kwa kamati yake, kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa..
Posted by MROKI On Thursday, April 11, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo