Nafasi Ya Matangazo

April 04, 2019

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WADAU wa sekta ya afya wameaswa kuimarisha ubia baina ya sekta ya umma na binafsi (PPP) mkoani Pwani, badala ya kusigana kwenye baadhi ya mambo ili kujiepusha kuweka rehani maisha ya wananchi ambao wanahitaji huduma bora ya afya .

Akitoa rai hiyo, wakati wa kikao kilichowakutanisha pande hizo mbili mjini Kibaha, mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliwaambia afya ni kitu muhimu kwenye maisha ya binadamu ili aweze kushiriki katika shughuli za kimaendeleo hivyo waondoe tofauti, kila mmoja kwa nafasi yake awe sehemu yake ili kutoa huduma.

Alieleza ,mkoa huo una jumla ya vituo vya kutolea huduma ya afya 342 ,kati ya hivyo 275 ni vya umma, 33 binafsi na 34 vya mashirika ya dini lakini ni vituo 20 vyenye malengo ya kuingia mkataba wa utoaji huduma ambapo sita pekee ndio vilivyoingia mkataba. 

"Kutokana na hali hii, manake kuna baadhi ya maeneo yanaathirika kwenye utoaji huduma kutokana na kutokuwa na makubaliano ya sekta ya umma na binafsi "anasema. Ndikilo alifafanua, asilimia 20 ni vituo vya binafsi mkoani humo na asilimia 80 ni vya umma hivyo bado kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuboresha huduma hizo. 

Aidha aliwataka wadau hao, kukutana kila mwaka ili kutathmini, kusimamia utekelezaji na mwenendo wa ubia baina ya sekta hizo. 

Nae mratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi Pwani, Dk. Hussein Athuman alibainisha lengo la kukutana ni kujenga mahusiano baina ya pande hizo, kubadilishana uzoefu na kujiwekea mikakati itakayosaidia kuleta chachu ya mabadiliko chanya kwenye sekta ya afya. 

Awali Dk. Mariam Ongara kutoka wizara ya afya alielezea, vituo vya kutolea huduma ya afya binafsi na mashirika ya dini vina mchango mkubwa kwa jamii. Mariam alisisitiza serikali inatambua mchango unaotolewa na sekta binafsi kwani ina mchango mkubwa kwa watanzania.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo
Posted by MROKI On Thursday, April 04, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo