Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Mkoani Tanga (Tawla) Mwanaidi Kombo
akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya sheria katika masuala ya ardhi na
jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga yaliyoandaliwa na chama
hicho
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga Wakili Latifa
Ayoub akizungumza wakati wa wa mafunzo ya sheria katika masuala ya ardhi
na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga yaliyoandaliwa na chama
hicho
Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Kisiwani wilayani Muheza
Mwansiti Bashiru akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo wakimsikiliza muwezeshaji.
Washiriki wakipata picha ya pamoja mara baada ya kumalizika
mafunzo hayo
MFUMO dume, mila kandamizi kwa wanawake kwenye kumiliki ardhi vimetajwa
kuchangia kwa asilimia kubwa upotevu wa haki zao katika jamii
zinazowazunguka.
Hayo yalisemwa na Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Mkoani Tanga
(Tawla) Mwanaidi Kombo wakati wa mafunzo ya sheria katika masuala ya
ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga.
Alisema vikwazo vingine ni mila za kibaguzi kwa wanawake ambazo
zimechangia kwa asilimia kubwa upotevu wa haki za wanawake hasa kwenye
kumiliki ardhi na kujikuta wakishindwa kupata haki yao ya msingi.
“Kwa kuliona hili na ndio maana sisi kama Tawla kumeamua kutoa mafunzo
ya kuongezea uelewa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga kwa lengo la kuweza
kutambua haki zao na namna ya kuweza kuzidai inapotokea “Alisema
Alisema licha ya hivyo lakini pia wameamua kuanza kutoa elimu kwa kundi
la wanawake ikiwemo kuanzisha klabu mbalimbali za mashuleni lengo likiwa
ni kuwaoa elimu wanafunzi ili waweze kujua haki na kuweza kupunguza
ubaguzi kwenye jamii.
Awali akizumza mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mkazi wa Bweni
wilayani Pangani Mwajuma Ally alisema wanashukuru kupata elimu hiyo
ambayo imewafungua kuweza kutambua haki zao na namna ya kuweza kuzidai
kwa kutumia sheria.
Mwajuma alisema awali walikuwa hawatambua wapi wanaweza kwenda kudai
haki zao wakati wanapokumbana na changamoto kwenye ndoa hususani
yanapokuwa yakijitokeza matatizo mbalimbali.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamewashirikisha washiriki kutoka wilaya za
Pangani, Tanga na Muheza ambao kwa pamoja wanapewa elimu katika masuala
ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake.
0 comments:
Post a Comment