Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongoza kikao kazi
ngazi ya Mawaziri kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili
masuala ya Muungano ikiwa ni kikao cha utangulizi kabla ya kikao cha Kamati ya Pamoja
kitakachoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan. Kikao hicho kimehudhiriwa pia na Manaibu Waziri na Makatibu
Wakuu wa Tanzania Bara na Zanzibar
Waziri Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akichangia katika kikao kazi
cha Mawaziri wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kujadili masuala ya Muungano.
Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu Bunge Ajira na Watu
wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu – Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki.
Sehemu ya Wajumbe wa kikao
hicho ambao ni Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakifuatilia kikao hicho, kilichofanyika katika
Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment