Nafasi Ya Matangazo

February 22, 2019

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma na mjumbe wa bodi ya TAPANET Mh Fatuma Toufiq aikichangia hoja , katika mkutano wa mwanzo wa mwaka unaowakutanisha washiriki kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar kwa lengo la kutadhimini mafanikio ya mradi changamoto na mikakati ya kutoa msaada wa huduma za kisheria baada ya 2020
Meneja uwezeshaji (capacity development ) wa LSF, Bwn Bryceson Munuo akiongea na wakuu wa bodi na mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria yanayofadhiliwa na LSF, katika mkutano wa mwanzo wa mwaka unaowakutanisha washiriki kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar kwa lengo la kutadhimini mafanikio ya mradi changamoto na mikakati ya kutoa msaada wa huduma za kisheria baada ya 2020
 Ofisa Mkuu wa LSF , Kees Groenendijk akitoa cheti cha utendaji bora kwa mwakilishi wa kibondo Paralegal kutoka mkoa wa Kigoma bwana Japhet  kufatia utendaji bora katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa mwaka 2018. Akishuhudia ni Meneja uwezeshaji (capacity development ) wa LSF, Bwn Bryceson Munuo
Ofisa Mkuu wa LSF , Kees Groenendijk akitoa cheti cha utendaji bora kwa Mkurugenzi wa CCT Cotrida Ndezi Kwa niaba ya Paralegal kutoka mkoa wa Dodoma, Katuka Paralegal Organisation Chamwino, kufatia utendaji bora katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa mwaka 2018. Akishuhudia ni paralegal kutoka katuka Chamwino bi Shida Andrea Sasine Meneja uwezeshaji (capacity development ) wa LSF, Bwn Bryceson Munuo.
************************
Wakuu wa Mashirika yanayojishughulisha na utoaji wa msaada wa kisheria wanakutana Dodoma kujadili mbinu stahiki za kupanua wigo wa utoaji wa huduma za kisheria nchini---lengo kuu likiwa ni kuwakwamua watanzania maskini kutoka katika matatizo mbalimbali ya kisheria na kuwasaidia kupata haki zao.

Kongamano hili inawakutanisha pamoja wakurugenzi na wajumbe wa bodi kutoka katika mashirika ya msaada wa kisheria yanayotekeleza miradi ya huduma za kisheria maeneo mbalimbali nchini chini ya ufadhili wa Shirika la Legal Services Facility (LSF).

“Mkutano huu unatoa fursa kwa wadau wa utoaji wa huduma za kisheria, hasa wale wanafadhliwa na LSF, kujadili mafanikio, changamoto mbalimbali na njia bora za katika utoaji wa huduma za kisheria na namna na kufikisha huduma za kisheria kwa watanzania wengi wahitaji, hasa waishio vijijini,” kwa mwaka 2018 tumeweza  kufikia watu zaidi ya million 3 kulinganisha na mwaka 2017 ambapo watu milioni 1 na laki 4 walifikiwa katika kupata elimu ya sheria. 

Na kwa upande wa msaada wa kisheria mwaka 2018 tumefikia idadi ya watu 76,000 kulinganisha na mwaka 2017 ambapo 65000 walifikiwa, ni wazi kabisa kumekuwa na ongezeko katika kuwafikia  na kubadili mtazamo,maisha ya wananchi kwa kuwawezesha kupata stahiki zao kwa maendeleo bora ya kijamii na kiuchumi  kila mwaka  amesema Meneja Mradi wa LSF-Ramadhan Maselle, wakati wa ufunguzi Mkutano huu.

Lengo kuu la Kangamano, kwa mujibu wa Maselle, ni kuhakikisha huduma za kisheria na wasaidizi wa kisheria zinawafikia watanzania wengi wenye matatizo ya kisheria, mpaka chini kabisa katika ngazi za vijiji.

Washiriki wa mkutano pia watapata nafasi kujadili kwa mapana na marefu mrradi wa LSF, mbinu za kufanya miradi/shughuli inayotekelezwa na vituo vya msaada wa kisheria, mashirika na wadau mbalimbali chini ya ufadhili wa LSF, iwe enderevu.

“Uenderevu wa miradi ni jambo la msingi sana, ndo maana kauli mbiu ya Kangamano hili la 2019 ni ‘LSF Grantees beyond 2020; Strengths and Challenges—maana yake Mashirika yanayofadhiliwa na LSF baada ya 2020; Uwezo na Changamoto. Kauli mbiu hii inatatoa fursa kwa LSF, mashirika yanayofadhiliwa na LSF na wadau wengine, kujadili mbinu mbadala za kuhakikisha shughuli na miradi ya usaidizi wa kisheria na utoaji wa huduma za kisheria, inakuwa enderevu hata kama ufadhili wa  LSF hautakuwepo,” kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na LSF.

“Mijadala na mikakati utokanayo na Mkutano huu yataisaidia LSF, mashirika yanayofadhiliwa na LSF na wadau wengine kupata uelewa mpana kuhusu mbinu mbadala zitakazosaidia kupata fedha na raslimali fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali mbadala kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya usaidizi wa kisheria na hatimae kuwakwamua watanzania maskini kutoka katika matatizo mbalimbaili ya kisheria yanayowakabili,”  alisisitiza Masele

Aidha katika Kangamano LSF itatoa vyeti vya utendaji bora kwa vituo 8 vya watoa huduma za msaada wa kisheria ambao wamefanya vizuri katika mwaka 2018. Vitu hivyo ni pamoja na Kibondo Kigoma , Makete Njombe, katuka Dodoma, toje tanga, kyela Mbeya, ukerewe Mwanza, Serengeti mara na Micheweni Zanzibar

Mkutano huu unatarajia kuudhuriwa na washiriki wapatao 106, ikiwa ni pamoja na viongozi wa mashirika yanayofadhiliwa na LSF, wajumbe wa bodi wa mashirika husika, viongozi wa serikali kutoka katika wizara mbalilimbali--TAMISEMI, Wizara ya Sheria na Katiba, Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, na waandishi wa habari.
Posted by MROKI On Friday, February 22, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo