Nafasi Ya Matangazo

January 28, 2019

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (pichani) amewataka  Wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuacha kulalamika kuhusu miundombinu ya shule wakati wanashindwa kutumia vyema fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo elekezi kuhusu utekelezaji wa Programu ya lipa kukingana na Matokeo katika sekta ya Elimu ambapo amewataka watendaji wa halmashauri kuacha kufanya matumizi tofauti na maelekezo yanayotolewa na kama upo ulazima wa kubadili matumizi halmashauri zinapaswa kuomba kibali cha kubadili matumizi na hawatatakiwa kuanza matumizi kabla ya idhini kutolewa.

“ Mpango huu wa lipa kulingana na Matokeo unekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi Cha kuanzia mwaka 2014/2015 hadi 2017/2018 halmashauri zimekuwa  zikifanya vizuri katika utekelezaji wa vigezo na hivyo kupata ongezeko la fedha kila mwaka kutoka Shilingi bilioni 15.53 (2014/2015) hadi kufikia shilingi bilioni 50 kwa mwaka ( 207/1018),”alisema Waziri Ndalichako.

Pia Waziri Ndalichako amewataka Wakurugenzi, Maafisa Elimu na Wathibiti ubora wa shule kuimarisha mfumo wa menejimenti na upatikanaji wa taarifa /Takwimu za Elimu na kuhakikisha kunakuwa na usawazishaji wa ikama ya walimu ndani ya halmashauri

Lengo la programu ya lipa kulingana na matokeo ni kuinua ubora wa Elimu nchini na kuwa fedha kupitia programu hii hutolewa kutokana na kukidhi vigezo vilivyokubalika na kufanyiwa uhakiki ili kuthibitisha kuwa vimetekelezwa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyija katika mikoa yote nchini.
Posted by MROKI On Monday, January 28, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo