Nafasi Ya Matangazo

January 26, 2019

Serikali imekamilisha miundombinu yote muhimu ikiwemo Maji, umeme na barabara kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa Chuo Cha Ufundi stadi VETA mkoani Kagera.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako baada ya kuzindua chanzo Cha Maji ambacho kitatumika kwa ajili ya kujenga  VETA hiyo katika kijiji Cha Burugo, Kwenye halmashauri ya Bukoba.

“Dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo mwaka 2025 ili kutimiza malengo hayo ndiyo serikali imewekeza zaidi katika kujenga vyuo vya Ufundi stadi ili kuwa na wataalamu wa kati na wa kutosha watakaotumika kwenye viwanda hapa nchini,”alisisitiza Waziri Ndalichako.

Awali akipokea taarifa ya mkoa huo kuhusu sekta ya Elimu, Waziri Ndalichako ameonesha kutoridhishwa na hatua za ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi mkoani humo na kuzitaka mamlaka husika kutafuta ufumbuzi ili kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi.

Waziri Ndalichako pia alitembelea Shule ya Bukoba Sekondari ambayo paa za shule hiyo ziliezuliwa kufuatia mvua kubwa Iliyoambatana na upepo na hivyo kulazimika wnafunzi wa shule hiyo kuhamishiwa katika shule ya sekondari Ihungo na wengine katika shule ya Sekondari omumwani.
 Moja ya majengo yanayojengwa
 Waziri Prof Joyce Ndalichako akikagua ujenzu wa chuo hicho. 
 Akitembezwa maeneo mbalimbali ya ujenzi.

Posted by MROKI On Saturday, January 26, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo