Nafasi Ya Matangazo

January 28, 2019


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto), akiwa na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo anayeshughhulikia usambazaji na huduma kwa wateja, Mhandisi Raymond Seya, (wakwanza kulia), Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona, wakati akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya wahariri wa vyombo vya habari waliokuwa wakitembelea mradi wa ukarabati na uimarishaji miundombinu ya umeme, TEDAP, na ule wa Kenya-Tanzania Power Interconnection Project (KTPIP) TII jijini Arusha.
 Dkt. Mwinuka na wasaidizi wake, wakiwa na wahariri.
Dkt, Mwinuka akisikilzia kwa makini maoni na maswali kutoka kwa wahariri

 Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Stella Hiza, akijitambulisha.
*************
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Arusha
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO Dkt. Tito Mwinuka amesema ndoto yake kama kiongozi wa shirika hilo ni kuona linajiendesha kwa faida.
Huu ni mwaka wa pili shirika letu linaendeshwa bila ruzuku ya serikali, miaka miwili au mitatu hapo nyuma ukichukua wastani tulikuwa tunapokea ruzuku ya wastani wa bilioni 200 kwa mwaka, kuna mwaka tulipata 400 na kitu na tukapata 358 lakini hiyo yote sasa hivi haipo tena tunajiendesha bila ya ruzuku ya serikali. Alibainisha.

Akieleza zaidi Dkt. Mwinuka alisema huo ndio uelekeo ambao angependa kuushuhudia akiwa TANESCO kwamba wanaendelea kuishi bila ruzuku, shirika linatengeneza faida na kutoa gawiwo kwa serikali ndiko ambako shirika linaelekea lakini pia kulipa madeni yote ya nyuma.

“Kwa historia TANESCO tumekuwa na madeni makubwa kutokana na hali mbaya hapo nyuma na madeni haya sasa yamesimama hayaongezeki, na deni likisimama haliongezeki ni dalili kwamba tutaanza kulilipa.” Alisema.

Alisema Shirika litaendelea kufanya miradi yake sambamba na kulipa madeni.
Aidha Dkt. Mwinuka alisema katika historia ya nchi hii, Serikaki kupitia TANESCO imeweza kutekeleza miradi mingi mikubwa ya umeme kwa wakati mmoja
“Katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya umeme kama nguzo ya muhimu ya ujenzi wa Tanzania yenye viwanda, Serikali kupitia TANESCO hivi sasa inatekeelza miradi mikubwa ya umeme 22 kwa wakati mmoja na kwa fedha za Serikali.”

 Alisema. Miradi hii inalenga kusogeza miundombinu katika maeneo ambayo hayajafikwia na umeme, lakini pia kukarabati miundombinu iliyochakaa au kuzidiwa katika maeneo ambayo yalishafikiwa na umeme. 
Posted by MROKI On Monday, January 28, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo