Nafasi Ya Matangazo

August 31, 2018

 Wiki ya Zimamoti na Uokoaji inataraji kumalizika leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo wadau mbalimbali wakiongozwa na jeshi la Zima Moto na Ukoaji wameshiriki katika maonesho yaliyoenda sambamba na utoaji elimu ya majanga ya moto na uokoaji.

Shirika la Umeme Nchini TANESCo ni miongoni mwa wadau waliounga mkono maaonesgo hayo yakwanza kuanza kufanyika mwaka huu.

Tanesco imetumia maonesho hayo kutoa elimu kuhusiana na huduma zao wanazotoa lakini kubwa zaidi likiwa ni elimu ya namna ambavyo umeme unaweza kusababisha ajali ya moto na kuteketeza nyumba na majengo.

Mhandisi wa Shirika Hilo anaeshughulika na Afya na Usalama mahali pa kazi, Donart Makingi amesema kuwa yapo mambo ambayo yanaweza kusabnabisha hitilafu katika jengo au nyumba ambavyo ni pamoja na matumizi ya vifaa vya umeme visivyo na ubora, utumiaji mafundi vishoka katika unganishaji umeme, vifaa visivyo na ubora. 

Lakini pia alisema kutumia vitu kama pasi au jiko bila uangalifu na umakini navyo vinaweza kuchangia hitilafu ya umeme na baade nyumba na mali zingine kuteketea. 
Wanafunzi ni miongoni mwa watu waliopatiwa elimu katika Banda la Tanesco.
Maofisa wa Tanesco kutoka idara mbalimbali wapo uwanjani kuhudumia mamia ya wananhi wanao tembelea.
Tanesco inawakumbusha wananchi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mifumo ya umeme walau kila baada ya miaka kadhaa ili kujua kama bado ipo sahihi, 
Posted by MROKI On Friday, August 31, 2018 No comments

August 30, 2018

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia) na Kamishna Jerenali wa Zimamoto, Thobias Andengenye wakisikiliza maelezo kutoka kwa ofisa Mwamdamizi wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi juu ya huduma za anuani za makazi zinavyoweza kusaidia utoaji haraka wa huduma za zima moto na uokoaji nchuni. Waziri Lugola alikuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya Zimamoto Nchini, iliyozinduliwa Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni miongoni mwa taasisi za serikali zilizoshiriki katika maonesho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji kitaifa ambayo inafanyika jijini Dodoma kwa mara ya kwanza nchini.

Lengo kuu la maadhimisho hayo ni kutoa elimu juu ya namna bora ya kuepuka majanga ya moto na kuwawezesha wananchi kuzifahamu vyema shughuli nyiongi zinazofanywa na jeshi hilo ambazo si tu kuzima moto kama inavyofahamika na wananchi wengi lakini ni pamoja na kusaidia katika majanga mbalimbali na ajali.

TCRA kama mdau mkubwa wa zimamoto mbali na kusaidia katika mawasiliano baina ya wananchi na Jeshi la Zimamoto kuwa rahisi na ya bure kwa mujibu wa sheria lakini pia kupitia mradi wao wa anuani za makazi unasaidia Jeshi hilo na wananchi kuweza kufikiwa kirahisi.

Ofisa Mwandamizi Mkuu wa Mawasiliano, Mabekl Masasi alimwambia Waziri Kangi lugola kuwa kupitia anuania za makazi zimeweza kurahisisha jeshi hilo kufika katika maeneo mengi kirahisi kwa kutaja jina la mtaa na namba ya nyumba la eneo husika. 
 Waziri wa Mambi ya Ndani, Kangi Lugola akiuliza jambo katika banda hilo la TCRA 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia) na Kamishna Jerenali wa Zimamoto, Thobias Ndengenye wakisikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) juu ya huduma za anuani za makazi zinavyoweza kusaidia utoaji haraka wa huduma za zima moto na uokoaji nchuni. Waziri Lugola alikuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya Siku ya Zimamoto Nchini, Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma jana.
Wananchi na maofisa mbalimbali wa Jeshi la Zimamoto wakiwa katika Banda la TCRA kupata vipeperushi na maelezo mbalimbali ya kazi za taasisi hiyo.
Posted by MROKI On Thursday, August 30, 2018 No comments

August 16, 2018

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley ,Jensen Natal akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya kabla ya kuingia katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiangalia pasi ya kusafiria ya anayedaiwa kuwa mwekezaji wa katika shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Trevor Robert raia wa Zimbabwe ambalo anatajwa kutokuwa na uhalali wa kuwa mwekezaji wa shamba hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo walipotembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate linatajwa kuwa na mwekezaji asiye halali. 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akimsikiliza Meneja wa Shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Trevor Robert wakati akitoa maelezo ya uhalali wa kuwekeza katika shamba hilo.
Askari Polisi wakiwa wamemshikilia ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley Tanzania,Jensen Natal inayotajwa kukwepa kulipa kodi ya serikali kutokana na uwekezaji katika shamba la Kibo and Kikafu Estate,Natal amekamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai.
Askari akimsindikiza Mwanasheria wa kampuni ya Tudeley Tanzania,Edward Mroso baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya TudeleyTanzania,Jensen Natal na Mwanasheria wa kampuni hiyo,Edward Mroso wakiwa kwenye gari la Polisi muda mfupi baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.

Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo baada ya kutembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazin.
MKUU wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa na kuwekwa rumande kwa saa 48 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudi inayomiliki Shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Jensen Natal pamoja na Manasheria wa kampuni hiyo,Edward Mroso.

mbali na kukamatwa kwa atu hao,Mkuu huyo wa wilaya ameamuru kushikiliwa kwa muda kwa Pasi ya kusafiria ya anayetajwa kuwa mwekezaji wa Shamba la Kibo and Kikau Estate,Trevor Robert kutokana na tuhuma za kukwepa kulipa kodi ya serikali inayokadiliwa kuwa Zaidi ya Sh Mil 700.
Posted by MROKI On Thursday, August 16, 2018 No comments
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akitamburishwa baadhi ya viongozi walioshiriki mkutano mkuu wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa J.K Nyerere uliopo Chuo Kikuu cha Ushirika,Moshi (MOCu) kwa ajili ya kufungua mkutano wa Tano wa chama hicho.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.
\Baadhi ya Wajumbe wakiwa katika mkutano huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Posted by MROKI On Thursday, August 16, 2018 No comments
Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeimarisha mkakati wake wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

Katika kutimiza hilo kampuni hiyo imekabidhi ofisi na bajaji tisa kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam na inatarajia kupanua mradi huo kwenda mikoa mingine ikiwemo Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma.

Akizungumza katika makabidhiano ya Bajaji hizo yaliyofanyika leo Alhamisi Agosti 16 katika makao makuu ya MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo Salum Salum, amesema hii ni awamu ya kwanza ya mradi huo ambapo wametoa jumla ya bajaji 27 kwa viunga 9 vya Dar es salaam na kwamba baada ya awamu hii watafanya tathmini na kisha kuupanua hapa Dar es Salaam ni mikoa mingine.

Amesema katika mradi huo, MultiChoice inawafadhili vijana hao ofisi za uwakala wa DStv na pia inawadhamini vitendea kazi muhimu kama vile Kompyuta na Bajaji ili viwawezeshe kufanya kazi zao kwa ufanisi.

2
 Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mmoja wa mawakala wapya wa mauzo wa DStv wa kiunga cha Temeke Rose Haule wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

“Tumekuwa tukifanya kazi na vijana wengi ambao ni mawakala wa mauzo wa kujitegemea (direct sales) lakini sasa tumeamua tuwafanye wabia wetu wa kibiashara na kuwawezesha kuendesha biashara rasmi ya uwakala wa DStv” alisema Salum na kuongeza kuwa vijana hao watakuwa wakitoa huduma katika maeneo maalum yajulikanayo kama ‘viunga’. Kila wakala atakuwa na kiunga chake, na atakuwa na jukumu la kuhakikisha wateja wa eneo lake wanahudumiwa kwa haraka

“Vijana hawa watakuwa na mtandao wa vijana wengine wa mauzo na mafundi wa kufunga DStv ambao wamepata mafunzo maalum na kuthibitishwa. Kwa hiyo, kama mteja yuko Mbagala, atahudumiwa na wakala wa kiunga cha Mbagala, hivyo hivyo aliyeko Tabata atahudumiwa na kiunga cha Tabata na hii itakuwa kwa viunga vyote ambavyo ni Mbagala, Tabata, Kigamboni, Ilala, Chang’ombe, Mbezi beach, Mbezi Kimara, Manzese na Ukonga.
3
Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum (wa pili Kulia) akizungumza na kiongozi wa Kiunga cha DStv Temeke Rose Haule (wa pili Kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj). Kulia ni Khalfani Soni na kushoto ni Omari Ali wote wa Gongo la Mboto.

Amesema kwa kuwarasimisha vijana hawa, sasa watakuwa wanafanya biashara rasmi, wakiwa na leseni na ofisi na hivyo kuweza pia kulipa kodi stahiki kwa serikali na hivyo kuongeza mchango wao kwa uchumi wa nchi.

Wakizungumza bara baada ya kukabidhiwa bajaji hizo sambamba na laptop, wakuu wa viunga hivyo wamesema wamekuwa wakifanya kazi kama mawakala wadogo wa kujitegemea kwa muda sasa lakini walikuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kutokuwa na ofisi rasmi na pia vitendea kazi hususan usafiri.

“Tulikuwa tunafanya mauzo kwa tabu sana kwani kwanza kutokuwa na ofisi ilikuwa ni vigumu kwa wateja kutupata. Pia hata ukipata mteja unalazimika kubeka vifaa kwenye usafiri usio wa uhakika kwenda kwa mteja na hii ilikuwa inapoteza muda na kuongeza gharama” alisema Rose Haule mkuu wa kiunga cha Temeke.
5
Wakala wa mauzo wa DStv Rose Haule wa Temeke (aliyeko ndani ya Bajaji) akifurahia na wenzake Khalfani Soni wa Gongo la Mboto,  Omari Ali wa Gongo la Mboto  na Sarah Makasia wa Manzese wakifurahia muda mfupi baada ya hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

Naye Yusuph Migeto wa kiunga cha Mbagala amesema kuwa kuwepo kwa ofisi na usafiri wa uhakika kutawahakikishia wateja wao huduma ya haraka na yenye ufanisi. “wakati mwingine wateja walikuwa wanalalamika kwa kucheleweshewa huduma kwani ukipata mteja inabidi ufuate vifaa DStv kisha uende kumfungia mteja. Hii ilikuwa inachelewesha sana. Lakini kwa sasa tutakuwa na uwezo wa kuwa na vifaa karibu na pia kuwepo kwa usafiri wa uhakika kutatufanya kufanya kazi kwa haraka zaidi
Posted by MROKI On Thursday, August 16, 2018 No comments

August 10, 2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha albamu ya picha Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt inayoonesha Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyobomolewa kabisa na tetemeko la ardhi Setemba 10, 2018  ambayo imejengwa upya na serikali ya Uingereza kupitia mpango wake wa maendelo ya elimu kupitia UKAid/DFID. Picha hizo zinaonesha shule hiyo baada ya tetemeko, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi siku ya mwaka mpya wa 2017 na inavyoonekana sasa baada ya kujengwa upya. Mhe. Mordaunt, ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi, alimtembelea  Rais Dkt. Magufuli akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018
Uingereza imetoa msaada wa shilingi Bilioni 307.5 kwa Tanzania kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika elimu, mapambano dhidi ya rushwa na uboreshaji huduma za afya.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ametangaza msaada huo leo tarehe 10 Agosti, 2018 alipokutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Penny Mordaunt amesema fedha hizo zinatolewa kwa ajili ya kuunga mkono vipaumbele vya Mhe. Rais Magufuli ambapo kati yake shilingi Bilioni 124.5 zitaelekezwa katika kuinua ubora wa elimu hususani kutoa fursa ya elimu kwa watoto wa kike na wenye ulemavu, shilingi Bilioni 23.5 zitaelekezwa katika kuunga mkono juhudi za kupambana na rushwa, na shilingi Bilioni 160 zitaelekezwa katika kuboresha huduma za afya.

“Tunafanya hivi ili kudhihirisha dhamira yetu ya kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wetu, tunataka kujielekeza katika kuhakikisha Mhe. Rais Magufuli anafanikisha ahadi zake kwa Watanzania na tunafurahi kuwa wadau muhimu wa hilo” amesema Mhe. Penny Mordaunt.

Ameongeza kuwa pamoja na kuwa wachangiaji wakubwa katika bajeti ya Serikali, Uingereza ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania na kwamba wanafurahishwa na wito wa Mhe. Rais Magufuli kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara zaidi kutoka Uingereza watakaowekeza kwa manufaa ya pande zote (win-win).

Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Penny Mordaunt kwa msaada huo na amemuomba kufikisha shukrani zake kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Theresa May kwa mchango mkubwa ambao Uingereza hutoa kuchangia bajeti ya Serikali na kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Namshukuru sana Waziri Penny Mordaunt kwa kutambua juhudi zetu za kuinua elimu, kupambana na rushwa na ufisadi pamoja na kuboresha huduma za afya, msaada huu utatusaidia kuongeza nguvu kwa sababu watoto wakipata elimu bora, tukikomesha rushwa na watu wetu wakiwa na afya njema tutaweza kujenga viwanda na kukuza uchumi wetu kwa kasi zaidi” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amemuahidi Mhe. Penny Mordaunt kuwa fedha zilizotolewa kiasi cha shilingi Bilioni 307.5 zitatumika vizuri na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha uhusiano wa Tanzania na Uingereza unazidi kuimarishwa kwa kuwa inatambua kuwa Uingereza ndio mwekezaji mkubwa hapa nchini na imekuwa ikitoa misaada mikubwa ya fedha za walipa kodi wa Uingereza kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.

Pia, Mhe. Rais Magufuli amemkabidhi Mhe. Penny Mordaunt albamu ya picha za shule ya sekondari Ihungo mkoani Kagera iliyojengwa upya baada ya kuharibika vibaya kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 2016, na ameishukuru Uingereza kwa msaada wa shilingi Bilioni 6zilizotumika kujenga majengo hayo kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ambaye amesema ziara ya Waziri Penny Mordaunt imezidi kukuza uhusiano wa Tanzania na Uingereza.

Posted by MROKI On Friday, August 10, 2018 No comments
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Likunja Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne, Agosti 10.2018 (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Likunja Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne, Agosti 10.2018 
 Wananchi wa kijiji cha Likunja wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliposimama na kuzungumza nao, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni tano katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Nanganga-Ruangwa yenye urefu wa kilomita 57 kwa kiwango cha lami.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Agosti 10, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Likunja wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi wilayani hapa.

Waziri Mkuu amesemaSerikali imeendelea kuboresha huduma za jamii nchini kwa kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo.

Amesema ujenzi wa barabara hiyo ya Nanganga-Ruangwa-Nachingwea hadi Masasi unatarajiwa kuanza hivi karibu, hivyo amewataka wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Akizungumza kuhusu nyumba zilizowekewa alama ya X, Waziri Mkuu aliwataka wahusika wazibomoe wenyewe ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa walivamia eneo na watakaosubiri hadi Serikali iwabomelee watalazimika kuilipia gharama, hivyo ni vema wakatii.

Wakati Huo huo,Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo asilimia 95 ya vijiji vyote vya wilaya ya Ruangwa vinapata huduma hiyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya wananchi wa kata hiyo kueleza changamoto zinazowakabili ikiwemo huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.

“Tumeendelea kuboresha huduma za jamii katika vijiji vyote vikiwemo na vya wilaya hii. mkakati wetu ni kuhakikisha wananchi wote mnapata maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yenu na tayari asilimia 95 ya vijiji vinapata maji,” amesema.

Kuhusu changamoto ya zahanati ya  kijiji cha Likunja kutokuwa na nyumba ya mganga, Waziri Mkuu amewashauri wananchi hao wafyatue matofali na kisha waanze ujenzi wa boma na Halmashauri itawasidia kuwapa vifaa vya viwandani kama saruji, mabati na misumari.
Posted by MROKI On Friday, August 10, 2018 No comments

August 04, 2018

 Maonesho ya Wakulima Nane Nane yamefunguliwa Agosti 3,2018 na Waziri wa Kilimo, Dk.Charles Mwijage na yanafanyika katika viwanja vya Nyakabindi vilivyopo nje kidogo ya Mji wa Bariadi (20km) Mkoani Simiyu na tayari wananchi wameanza kutembelea maonesho hayo na kujifunza na kuona vitu mbalimbali. 



















Posted by MROKI On Saturday, August 04, 2018 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo