Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2018




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina elekezi ya maofisa michezo ilifanyika katika Chuo Cha Mipango cha Dodoma. Semina hiyo ilihudhuriwa na maofisa michezo wa mikoa kutoka mikoa 26 ikiwemo na Zanzibar.

Baadhi ya maofisa michezo walioshiriki semina elekezi wakifuatilia hotoba ya Waziri Jafo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo, (Kushoto) akisalimiana na Meneja wa Chapa ya Cola-Cola nchini, Sialouise Shayo. Wengine pichani ni Maofisa wa Coca-Cola na Maofisa Michezo.

Maofisa wa Coca-Cola, Maofisa michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Mh.Jafo, (Katikati wa waliokaa) baada ya ufunguzi wa semina elekezi. 
 
Na Mwandishi Wetu. Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo,ameipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kuwekeza kudhamini mashindano ya Shule za Sekondari nchini ya UMISSETA kwa kipindi kingine mwaka huu na kuahidi kuwa serikali nayo pia itaendelea kuiunga mkono. 
 
Akifungua semina elekezi ya maofisa wa michezo kutoka mikoa 26 ya hapa nchini iliyofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki,ambapo pia aliambatana na Naibu Waziri wake, Joseph Kakunda, Waziri Jafo, alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa kampuni ya Coca-cola wa kukuza vipaji vya michezo kwa vijana. 
 
“Nimevutiwa sana na maandalizi na usimamizi wa mashindano ya michezo ya UMMISETA ulivyokuwa mwaka jana,kwa hili nawashukuru Coca-Cola,nafahamu kuwa mkataba wao ulikuwa wa kudhamini mashindano haya kuanzia mwaka 2015 hadi 2018,natoa wito kwao kuangalia uwezekano wa kuongeza muda wa udhamini ikibidi hata kuwa na haki ya kuyasimamia moja kwa moja,”alisema Jafo. 
 
Pia alitoa wito kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuweka mikakati itakayowezesha vilabu vya michezo vya hapa nchini kukuza vipaji vya mchezo wa soka vitakavyokuwa vimeibuliwa kupitia mashindano haya na kuwapatia wachezaji hao nafasi za kuendeleza vipaji vyao. 
 
Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo alisema “Lengo kuu la kampuni ya Coca-Cola ni kuwezesha vijana kushiriki katika michezo,kwa mara ya kwanza pia tutaifikia mikoa ya Tanga na Mtwara ambapo tutatoa jezi na vifaa vingine vya michezo” 
 
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda, alipongeza udhamini wa mashindano haya kutoka Kampuni ya Coca-Cola “Moja ya changamoto kubwa iliyopo ni jinsi ya kuendeleza vipaji vya michezo vinavyoibuliwa kupitia mashindano ya UMISSETA. Mrisho Ngassa, Juma Kaseja, Leodgar Tenga ni baadhi ya wanasoka ambao vipaji vyao viliibuliwa na mashindano haya”. 
 
Alitoa wito kwa serikali kuongeza juhudi za kuboresha mashindano ya UMISSETA ikiwemo kuhakikisha inatoa mafunzo kwa walimu wa michezo mashuleni sambamba na kuhakikisha kila manispaa nchini inatenga maeneo ya viwanja vya michezo. Semina elekezi ya makocha na maofisa michezo ilifanyika katika Chuo Cha Mipango cha Dodoma. 
 
Ilihudhuriwa na maofisa michezo wa mikoa kutoka mikoa 26 ya hapa nchini, ikiwemo Afisa Michezo kutoka Zanzibar,Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo la Taifa,Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Wajumbe wa Sekretarieti ya UMISSETA kitaifa. 
 
Kufanyika kwa semina hii pia ni uzinduzi rasmi wa mashindano ya UMISSETA 2018 uliofanywa na Waziri Jafo,mashindano haya ngazi ya kitaifa yatafanyika siku za baadaye katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Butimba mkoani Mwanza,na aliahidi kumuomba ,Mh.Rais John Magufuli,kuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wake.
Posted by MROKI On Tuesday, March 13, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo