Mratibu wa Mashindano ya Riadha ya Tanga City Marathon, Juma Mwajasho
kulia akitetea jambo na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya
kuelekea mashindano hayo Jumamosi wiki hiikushoto ni Meneja wa Mkwabi
Super Market ya Jijini Tanga ambao niwaandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab
Hussein na Katibu wa Chama cha Riadha Mkoani Tanga (RT) Hassan Mwagomba
Katibu
wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na uwepo wawashiriki kutoka Visiwa vya
Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapat afursa ya kuonyesha umahiri
wao kulia ni Meneja wa Mkwabi Super Marketya Jijini Tanga ambao ni
waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein,
Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo, Kawkab Hussein akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huu kuhusiana na zawadi zitakazotolewa msimu huu
Sehemu ya medali zitakazotolewa kwenye mashindano hayo
******************
MKUU
wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ametarajiwa kushuhudia mashindano ya
riadha ya Tanga City Marathon msimu wa piliyanayotazamiwa kufanyika
Jumamosi wiki hii mjini hapa.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Mratibu wa Mashindano hayo, Juma Mwajasho alisema maandalizi
yamekamilika kwa asilimia kubwa huku baadhi ya washiriki wakithibitisha
kushiriki.
Alisema katika mashindano hayo msimu huu watazamia
washiriki zaidi ya600 ambapo washindi watakabidhiwa zawadi mbalimbali
zikiwemo medali ambazo zimeandaliwa na wadhamini wa mashindano hayo.
Aidha alisema mashindano hayo yatashirikisha wakimbaji kwenye umbali wa
kilomita 21,10 na 5 ambapo wataanzia mbio hizo kwenye eneo la Mkwabi
Super Market kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini Tanga na kuishia eneo
hilo.
“Lakini kwa mara ya kwanza washiriki wote watakaoshiriki mashindano hayo watapewa medali na mgeni rasmi kwenye mashindano hayo.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan
Mwagomba alisema mashindano hayo pia yatashirikisha washiriki kutoka
Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapata fursa yakuonyesha
umahiri wao.
Alisema njia zitakazopitia mashindano hayo
zimeboreshwa zaidi kiusalama kwa wakimbiaji ili kuweza kuepukana na
adhari zinazoweza kujitokeza wakati yakiendelea.
Naye kwa
upande wake,Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni
waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein alisema msimu huo
wameboresha mashindano hayo kwa kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi
wa kumi.
Alizitaja zawadi zinazotolewa kuwa ni mshindi wa
kwanza km 21 atapata700,000 wa pili 500,000, huku mshindi wa tatu
akipata 300,000 huku wengine kuanzia wa nne hadi wa kumi watapata kifuta
jasho cha 50,000.
Hata hivyo alisema katika kilomita 10
mshindi wa kwanza atapata 250,000, wa pili 150,000 na wa tatu 100,000
huku washindi wa kuanzia nafasi ya nne mpaka 10 watapewa 30,000 pia
kutakuwa na vituo maalumu kwaajili ya kutoa huduma ya maji kwa
wakimbiaji (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
0 comments:
Post a Comment