MWANDISHI wa habari chipukizi wa vyombo vya habari vya Digital
vinavyomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) maarufu kama
Daily News Digital, Katuma Masamba (pichani) amefariki dunia.
Taarifa iliyotolewa na Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah
ilisema Katuma (24) alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Rufaa
ya Temeke mkoani Dar es Salaam, alikokimbizwa ili kupatiwa matibabu
baada ya kuugua ghafla juzi akishiriki Jukwaa la Biashara la TSN mjini
Zanzibar.
Mjomba wa marehemu, Shamte Ally alisema hospitalini hapo jana kuwa
mipango ya mazishi ya Katuma ambaye awali alikuwa mwandishi wa habari wa
gazeti la Habarileo, itafanyika baada ya kikao cha familia kukaa leo na hasa baada ya mama yake kufika.
Dada wa Katuma, ambaye ni mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji la
Taifa (TBC), Nyambona Masamba alisema ndugu wamepokea kwa mshituko
mkubwa taarifa za kifo hicho cha Katuma.
Taarifa zaidi kuhusu mazishi ya
Katuma, zitaendelea kutolewa kwa kadri mipango itakavyokuwa inakwenda.
Alfajiri ya leo Mjoba wa Marehemu Katuma, Shamte Ally alituma ujumbe mfupi kwa mmoja wa waandishi wa Gazeti tando hili la Daily News Online Blog, Mroki Mroki aliyeko Dodoma na kusema kuwa wanamsubiri mama mzazi wa Katuma anaewasili leo kwa maamuzi juu ya maziko ya mtoto wake.
Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa TSN, wanaungana na familia ya
marehemu katika wakati huu mgumu wa maombolezo.
0 comments:
Post a Comment