Washiriki wa Mkutano huo wakiendelea na mijadala
Na Mwandishi Wetu
WAZO la kutumia fursa ya faida ya kuthamini thamani katika sekta ya madini limeuteka mkutano wa bara la Afrika unaoendelea nchini Ghana uliojikita kujadili namna ya kuongeza thamani katika sekta ya Uchimbaji.
Wajumbe wa mkutano huo ambao ulianza jijini Accra, jana wamebainisha kuwa mataifa mengi ambayo yana utajiri mkubwa wa madini barani Afrika sio tu yana faidika kwa kiwango kidogo kutokana na rasilimali zao kupitia mauzo ya nje ya madini ghafi bali pia faida za ajira na suala la kuwajengea uwezo wa fedha limekuwa kidogo hivyo kuwafanya wawe wahanga wa kushuka kwa thamani ya masoko ya rasilimali duniani.
Akifungua mkutano huo wa siku mbili, Makamu wa Rais wa Ghana, Dkt. Mahamudu Bawumia, alisema kuwa Afrika ina asilimia 30 ya rasilimali za madini duniani, asilimia 12 ya hifadhi ya mafuta duniani na asilimia 42 ya hifadhi za dhahabu za dunia lakini bado umaskini unaendelea katika bara hili.
"Dhana ambayo tumekuwa tukiifanya ama kuiendeleza tangu kujipatia Uhuru inahitaji mabadiliko. Tumekwenda katika njia ya uchimbaji wa rasilimali za asili lakini hakuna faida.Hivyo, mtazamo mpya na mabadiliko yatahitaji kwa bara hili katika suala la kuuza nje bidhaa ghafi ," alisema
Dkt Bawumia alibainisha kuwa jambo hilo linawezekana kufanikiwa kupitia kuongeza thamani bidhaa zetu tunazouza nje badala ya kuziuza zikiwa ghafi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Utafiti na Sera katika Taasisi ya Uongozi, Dennis Rweyemamu, alisema Afrika ina wingi wa rasilimali za ziada lakini inakosa utaalamu wa kutengeneza madini hayo na kuyafanya yawe bidhaa zenye thamani kubwa.
" Madini mengi yanayochimbwa na kusafirisha kuzwa nje yana kuwa bado katika hali ya kuwa ghafi, na mchakato wa kuyaongezea thamani hufanyiki kwingineko , hivyo kufanya mataifa ya Kiafrika yenye utajiri wa madini yapate faidi kidogo kutokana na mauzo hayo ya rasilimali ghafi na pia kupunguza ajira faida za ajira na kufanya mataifa hayo utegemezi wa masoko ya rasilimali duniani. "Rweyemamu alisema.
Aliwaambia wajumbe kuwa katika nchi nyingi za kiafrika, uchimbaji wa rasilimali ni sekta inayojitenga kutoka katika shughuli nyingine za kiuchumi, na kuongeza kuwa kimsingi uzalishaji unaotumia mitambo zaidi umetoa nafasi finyu kwa nchi mwenyeji katika uzalishaji katika masuala ya ugavi na ajira .
"Hii inamaanisha kuwa katika sekta ya uchimbaji ya madini imeshindwa kuwa chanzo cha ukuaji wa uchumi kupitia kutengeneza ajira, mahitaji ya bidhaa za ndani na huduma pamoja na kutoa ujuzi na teknolojia kwa nchi husika ."
Pia alibainisha kuwa nchi zimekuwa zinategemea kupata mapato kupitia mirahaba, faida zitokanazo na hisa na makampuni , gawio kwa serikali uliofanyika usawa kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha alibainisha kuwa kwa sasa kuna ongezeka la ufahamu hivyo alisema, faida kubwa zaidi na endelevu inaweza kupatikana kutoka kwa kila gramu ya madini yanayochimbwa kupitia ongezeko la thamani.
0 comments:
Post a Comment