Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqqaro, akizungumza katika kipindi cha Goodmorning, kinachorushwa na kituo cha Matangazo cha Redio cha Redio 5 Arusha na kuwahimiza wakati wa Arusha kujitokeza katika uamdikishaji wa kupatiwa Vitambulisho vya taifa.
Mkurugenzi wa kituo cha Redio 5, Robert Francis akisalimiana na Afisa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Arusha Mjini, Juliette Raymond . Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Daqqaro.
Mkurugenzi
wa kituo cha Redio 5, Robert Francis (kulia), Afisa kutoka
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Arusha Mjini, Juliette Raymond wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Daqqaro.
Mkurugenzi
wa kituo cha Redio 5, Robert Francis akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Daqqaro.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqqaro amewataka
wananchi wa wilaya ya Arusha Mjini Kuchangamkia Uandikishwaji
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambalo linaendelea katika Kata tatu za Wilaya
hiyo.
Akizungumza katika kipindi cha Goodmorning Tanzania
kinachorushwa na kituo cha Matangazo cha Redio cha Redio 5 Arusha Daqqaro,
amesema kuwa zoezi hili lina manufaa makubwa kwa wananchi na watanzania kwa
ujumla lakini pia vitambulisho hivyo vitawawezesha watanzania kutambulika kila
mahala, pamoja na raia wa kigeni kufanya shughuli zao bila usumbufu ikiwa ni
pamoja serikali kuwa na taarifa sahihi za wananchi.
Aidha amesema kuwa wananchi wasisubiri mpaka zoezi hilo
kufikia tamati ndio kujitokeza Kwa wingi
kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha msongamano na usumbufu mkubwa
kwa wananchi.
“Naomba niwafahamishe na kutoa rai kwa wananchi wangu
wajitokeze kwa wingi katika zoezi hili na wasisibirie siku kubaki chache ndio
wajitokeze kwa kuwa kunapelekea usumbufu mkubwa sana hivyo,zoezi hili pia
litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi”alisema fabian
Pia ametaka kila
mwananchi kushiriki zoezi hilo na kutolihusisha na masuala ya kisiasa kutokana
na umuhimu wake,kwa kuwa lengo ni kutambua na kusajili na kutoa vitambulisho
vya taifa.
Afisa kutoka mamlaka hiyo wilaya ya Arusha Mjini Juliette Raymond Amesema lengo la zoezi hilo ni kuwezesha
serikali kutambua wananchi wake wapo wapi na wanafanya nini ilimradi anaishi ndani ya mipaka ya Tanzania ,hivyo
zoezi hilo ni lazima kwa kila mtu kwa
Mujibu wa sheria.
Kwa wilaya ya Arusha Mjini zoezi hilo linaendelea katika
kata ya Sombetini,Sekei na Themi ambapo zoezi hilo linafnyika katika
Halmashauri ya Jiji la Arusha katika kata ya Sekei,Themi katika viwanja vya
nane nane na Sombetini Ofisi za Mtendaji kata eneo la Mbauda Sokoni.
0 comments:
Post a Comment