Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage
Chande akitangaza punguzo kubwa la bei kwa vifurushi vyote vya DStv bei
zitakazoanza kutumika rasi Septemba mosi 2017.
*****************
Katika kuhakikisha kuwa wateja wake wote
na watanzania kwa ujumla wanaendelea kufurahia huduma za DStv, kampuni ya
Multichoice Tanzania imetangaza neema kubwa kwa wateja wake kwa kufyeka bei za vifurushi
vyake vyote, huku pia ikiboresha maudhui na vipindi katika vifurushi vyake
hususan vile vya bei ya chini!
Habari hiyo njema imetangazwa leo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, alipokuwa akiongea
na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
ambapo amesema bei hizo mpya zitaanza kutumika
rasmi Septemba mosi 2017.
“Kumjali na kumsikiliza mteja ni nguzo
ya uendeshaji wa biashara yetu. Tumesikia maoni ya wateja wetu na wananchi kwa
ujumla kutusihi tuangalie uwezekano wa kupunguza bei, tumechanganua kwa kina na
tumeamua kutekeleza matakwa yao, leo hii tumepitisha panga kwenye bei za
vifurushi vyetu vyote!” alisema Maharage.
Akifafanua kuhusu punguzo hilo, Maharage
amesema kumekuwa na punguzo la hadi
asilimia 16, ambalo ni punguzo kubwa sana na litakalowapa ahueni kubwa
watumiaji wa DStv. Amezitaja bei mpya kuwa ni;
Bei Mpya za vifurushi vya DStv:
Kifurushi
|
Bei ya sasa
|
Bei Mpya
|
% Ya Punguzo
|
Premium
|
TZS
184 000.00
|
TZS
169 000.00
|
8.15%
|
Compact
Plus
|
TZS
122 500.00
|
TZS
109 000.00
|
11.02%
|
Compact
|
TZS
82 250.00
|
TZS
69 000.00
|
16.11%
|
Family
|
TZS
42 900.00
|
TZS
39 000.00
|
9.09%
|
Access
(Bomba)
|
TZS
19.975.00
|
TZS
19 000.00
|
4.88%
|
Mara baada ya kutaja bei hizo Maharage
aliwaambia waandishi wa habari; “Kwa
lugha ya mtaani wanasema ‘Vuma Vimekaza’ – ikimaanisha hali ya kifedha imebana…
Multichoice imelisikia hilo na kuamua kuwapa wateja wote wa DSrv ahueni kubwa!
Sasa kwa wateja wetu wa DStv, ‘Vyuma vimeachia’”
Maharage amesisitiza
kuwa Multichoice itaendelea kuwasikiliza wateja wake na kuhakikisha kuwa
inatekeleza kile wanachohitaji wateja wake pale inapowezekana.
“Wateja wetu walituomba
tuongeze maudhui ya kitanzania kwenye king’amuzi chetu, tukawasikia, tukaweka chanel
maalum kabisa ya Maisha Magic Bongo ambayo ina asilimia 100 ya maudhui ya Kitanzania;
wakatuomba tupunguze bei ya vifurushi, tukafanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana,
na leo tena kwa mara ya pili tumepunguza bei, wakatuomba tuongeze chanel kwenye
vifurushi vya bei ndogo, tukafanya hivyo, tukaleta Laliga na Ligi kuu ya
uingereza hadi kwenye kifurushi cha chini kabisa cha Bomba”.
“Kipekee kabisa
Wananchi kupitia serikali wakatuomba tuongeze nguvu kwenye kuinua vipaji vya
vijana wetu wa kitanzania, tukasikia, tukaitikia, tukaanza katika riadha ambapo
tumemdhamini mwanariadha wetu Alphonce Simbu. Sote tunajua matokeo yake, sasa Tanzania
inahofiwa kwenye ulingo wa riadha kimataifa! Haya yote tumefanya kwa sababu
tunawasikiliza wateja wetu, tunawasikiliza wadau wetu, tunawasikiliza
Watanzania” alisema Maharage.
Wakati habari hii ikiwa
ni njema kwa watanzania wote, washabiki na wanazi wa kandanda wameonekana
kufurahia Zaidi kwani kwa punguzo hilo kuwa wataweza kushuhudia ligi kuu ya
uingereza PL pamaja na ligi nyingine kubwa ulimwenguni na makombe maarufu kama
UEFA kwa bei nafuu zaidi.
Kwa maelezo Zaidi
kuhusu bei mpya na vipindi mbalimbali katika vifurushi vya DStv tembelea; www.dstv.com.
0 comments:
Post a Comment