Nafasi Ya Matangazo

July 04, 2017

Kama ilivyo ada, King’amuzi cha DStv kitaonyesha mubashara mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Tanzania na Zambia ikiwa ni nusu fainali ya michuano ya COSAFA 2017 itakayochezwa kesho Jumatano saa 12 jioni huko Afrika Kusini
Taifa stars imefuzu nusu fainali baada ya shughuli pevu ya kuwafunga wenyeji Africa Kusini (Bafana Bafana) na sasa itakumbana na moja ya miamba ya soka barani Afrika Zambia katika nusu fainali inayotarajiwa kuwa na upinzania mkali.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria amethibitisha kuwa mechi hiyo itarushwa mubashara kupitia DStv chaneli ya SuperSport4 ambayo inapatikana kwenye vifurushi vyote kikiwemo kile cha DStv Bomba ambacho hupatikana kwa Sh 19,975 tu.
“Kwanza kabisa tunawapongeza sana Taifa Stars, wamefanya kazi kubwa, wameleta matumaini makubwa, sasa kazi ni moja tu, kwenda fainiali na sisi DStv, tunawahakikishia wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa mtanange huo watauona mubashara kupitia DStv” alisema Alpha.
Ameongeza kuwa enzi ya watanzania kusubiri matokeo ya michuano mikubwa kama hii ka saa kadhaa baada ya mechi kukamilika umepitwa na wakati, kwani kwa DStv, michuano hiyo huonyeshwa moja kwa moj. “Hakuna tena kwend amtandaoni kuangalia matokeo, wala kumuuliza mtu, ukiwa na DStv, unashuhudia mwenyewe” alisema.
Huduma za DStv zimekuwepo hapa Tanzania kwa miaka 20 sasa na maelfu kwa maelfu ya watanzania wameunganishiwa huduma za DStv na kuwafanya mamilioni ya watanzania katika kila pembe ya nchi kufurahia huduma zake. Mbali na kujikita Zaidi katika michezo na burudani, DStv pia ina chaneli mbalimbali za habari, Sanaa, Dini, Utafiri, Sayansi na Teknolojia, na pia utamaduni.
Posted by MROKI On Tuesday, July 04, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo