Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa
mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi 32 wa darasa la saba,
walimu 2 na dereva wagari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha
vilivyotokea leo saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata
ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Wanafunzi
na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo
Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo
la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni
ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu.
Kufuatia
ajali hii, Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Bw. Mrisho Gambo na kueleza kuwa ajali hiyo imezima ndoto za watoto
waliokuwa wakijiandaa kulitumikia Taifa na imesababisha uchungu, huzuni na
masikitiko makubwa kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla.
“Ndg
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo naomba unifikishie pole nyingi kwa
wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote wa wanafunzi, walimu na dereva waliopoteza
maisha, hiki ni kipindi kigumu kwetu sote, na uwaambie naungana nao katika
majonzi na maombi.
“Muhimu
kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone
haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu” Amesema
Mhe. Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment