Mwanariadha Alphonce Simbu (katikati) akipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA mkoani Kilimanjaro leo. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania
Johnson Mshana na Kushoto ni Meneja wa mwanariadha huyo Francis John
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha ambaye pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Iddy Kimanta akimpongeza Alphonce Simbu.
Balozi maalum wa DStv na Mwanariadha pekee wa
Tanzania liyeshiriki mashindano ya London Marathon Alphonce Simbu
amerejea nyumbani na kutoa onyo kali kwa wale atakaokabiliana nao kwenye
mashindano yajayo
ya dunia yatakayofanyika mwezi Agosti jijini London.
Simbu ambaye alishika nafasi ya tano katika
mashindano hayo na kujishindia kitita cha dola za marekani 10,000
aliwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kulakiwa
na maafisa mbalimbali akiwemo Meneja Uhusiano wa Multichoice
Tanzania Johnson Mshana, Meneja wa mwanariadha huyo Francis John
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika jijini Arusha muda mfupi baada ya yeye kuwasili Simbu
aliwashukuru sana watanzania wote kwa moyo wao na jinsi walivyomuunga
mkono na kumtakia kila la heri katika mashindano hayo.
Amesema alifarijika sana na pia kupata moyo zaidi alipokuwa akipokea
salamu kutoka kwa watanzania kote ndani nan je ya nchi.
Akizungumzia mashindano hayo, Simbu amesema
yalikuwa na changamoto kama yalivyo mashindano mengine makubwa ya
kimataifa kwani yalishirikisha vigogo ambao wengi wao wana uzoefu mkubwa
katika mashindano mbalimbali na wengine pia ni washindi
wa mashindano ya hapo awali.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye
aliwakilishwa na mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddy Kimanta alisema mkoa mzima wa
arusha umepokea kwa Furaha habari za mkazi wao kufanya vizuri katika
mashindano makubwa kama hayo na kwamba wataendelea kushirikiana
na Simbu na kumsaidia kwa kadiri itakavyowezekana ili kumuwezesha
kuendelea kuuwakilisha vizuri mkoa na taifa kwa ujumla kwenye michuano
ya kimataifa.
Amesema kuwa ushindi wa simbu uwe ni chachu kwa
vijana wengine wa kitanzania wenye vipaji na wasibaki nyuma bali
wajitokeze na watie nguvu katika kuonyesha vipaji vyao. “Tuna vipaji
vingi sana tena siyo kwa riadha tu, bali vya kila aina,
cha mshingi ni kushirikiana kwa karibu na wadau ili kuhakikisha vipaji
hivyo vinaibuliwa na kuendelezwa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla”
alisema mkuu huyo wa mkoa.
Naye Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania
Johnson Mshana amesema wao kama wadhamini wa Simbu wamepokea kwa Furaha
kubwa matokeo hayo ambayo yanaonyesha kuimarika kwa kiwango cha Simbu.
“Tuliamua kumdhamini Simbu tukiamini kabisa kuwa
atakuwa nyota na atailetea Tanzania sifa. Tuna dhamira kubwa nay a
dhati kabisa ya kuhakikisha kuwa siku moja wmbo wetu wa taifa unapigwa
katika mashindano ya Olimpiki. Bila shaka hili lipo karibu
kutokea”.alisema Mshana
Multichoice Tanzania inamdhamini Simbu kwa muda wa
mwaka mzima kwa lengo la kufanikisha maandalizi yake ya kushiriki katika
mashindano ya Dunia ya mwaka huu. Udhamini huu ulianza tangu mwaka 2016
ambapo Multichoice humpatia Alphonce posho
ya kujikimu pamoja na kusaidia kambi yake ya mazoezi.
Alphonce, ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda
medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai
Marathon, anatarajiwa kushiriki mashindano ya riadha ya dunia
yatakayofanyika London mnamo mwezo Agosti mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment