Na Bety Alex Arusha
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amefanya ziara ya kukagua miradi
ya maji,zahanati na barabara kwenye kata ya Kisongo tarafa ya mukulati
halmashauri ya wilaya ya Arusha mkoani Arusha iliyo lenga kutatua kero
na changamoto zinazo wakabili wananchi.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya zahanati ya
Engorora alisema kuwa serilika ya awamu ya tano imewekeza kwa wananchi
kwa asilimia kubwa ndio maana tunaona viongozi wanatoka maofisi kwenda
kusikiliza matatizo ya wanachi ili kutekeleza wajibu wao kulingana na
sera ya hapa kazi tuu ili kuweza kulikomboa taifa kuepukana na wimbi la
umaskini.
Gambo
alisema kuwa mabosi walio waweka madarakani ni wananchi hivyo viongozi
wanapaswa kushindana kupambana na kero za wananchi na wataakikisha
wanatatua na kutekeleza wajibu wao ili kuletea maendeleo ya kweli kwa
wananchi ili kutekeleza dhamira ya serikali ya Rais magufuli iliyo
lenga kuwajali wananchi wanyonge na wakipato cha chini ambapo alisema
serikali aitawafumbia macho viongozi wavivi,wazembe na wasio wajibika
kutekeleza wajibu wao .
Gambo
amewataka wananchi kufanyaka kazi kwa bidii hili kuepukana na wimbi la
umsikini ambapo itasaidia kujenga uchumi imara kwa wananchi kupata
uduma muhimu kwa haraka ilikuweza kujitegemea na kujenga uchumi imara
ambao taifa litaweza kufanya shughuli zao bila kutegemea misaada ya nchi
zingine duniani ambazo ziumekuwa zikisaidia kwenye sekta mbalimbali za
kielimu,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.
Wakizungumza
na Waandishi hapo juzi wananchi wa kijiji cha Engorora walisema kuwa
uhaba wa ukosefu wa maji kwa muda mrefu umesababisha wananchi kwenda
kutafuta maji kutoka bomba la jeshi la wananchi monduli [Jwtz] ambayo
yamekuwa yakitoka mara mbili kwa wiki jambo ambalo alitoshelezi maitaji
ya maji kwa wakaazi wa eneo hilo.
Walisema
kuna mradi wa maji unaofadhiliwa na benki ya dunia ambao umelenga kutoa
uduma kwa kijiji cha Loovilukuny ulioanza tangu mwaka 2o14 lakini bado
haujakamilika na gharama za mradi huo ni shilingi million 87,000,000/
ambao unasimamiwa na ofisi ya wilaya kama wakikamilisha kwa wakati
itapunguza kero ya maji kwa vijiji vya kata ya kisongo.
Sambamba
na hilo wananachi wa kata ya kisongo wamaendelea kupaza sauti kwa mkuu
wa mkoa kwenye suala la upatikanaji wa umeme vijijini [REA] bado
ujafikia vitongoji vingi kwa kipingi kilicho pita. “Tunaomba msukumo
wako mkuu wa mkoa ili kufikia utekelezaji wa awamu ya Tatu ‘ umeme
usambazwe katika vitongoji na kaya zote ususani katika maeneo ya huduma
za jamii kama shule, vituo vya Afya na zahanati “.
Aidha
wamemuomba mkuu wa mkoa kuongea na mamlaka ya ujenzi wa barabara,nyumba
na majengo [ TANROAD] ili kuweka matuta maeneo hatarishi katika
barabara kuu kwani ni hatari kwa wananchi wavukao kwa miguu eneo la
waya.
Arusha

0 comments:
Post a Comment