Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi,Richard M. Kayombo
UHAKIKI WA TIN DAR ES SALAAM
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru wananchi na wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ushirikiano walioutoa wakati wa zoezi la
kuhakiki Namba ya Utambulisho wa
Mlipakodi (TIN) kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo awamu ya kwanza ya zoezi
hili ilianza rasmi tarehe 16/08/2016 na kuhitimishwa tarehe 31/01/2017.
Hata
hivyo kutokana na sababu mbalimbali imebainika kwamba baadhi ya wananchi
walishindwa kukamilisha zoezi hilo katika muda uliopangwa.
Mamlaka
inapenda kuwatangazia wakazi wote wa Dar es Salaam kuwa wale wote wenye TIN
ambazo hazikuhakikiwa wanapaswa kutembelea ofisi za Mamlaka katika Mikoa yao ya
Kodi kwa maelekezo ya uhakiki.
Tunapenda
kusistiza kwamba wahusika watalazimika kuhakiki taarifa zao kabla ya kupata
huduma zifuatazo:
1.
Kulipia
ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazotoka na kuingia Nchini
2.
Kuhuisha
leseni za udereva
3.
Kulipia
ada ya mwaka ya gari
4.
Kulipa
kodi nyinginezo zinazosimamiwa na Mamlaka
5.
Kupata
cheti cha uhalali wa ulipaji kodi (Tax
Clearance Certificate)
Kwa
wananchi walioko nje ya nchi kwa sababu mbalimbali katika kipindi cha uhakiki,
wanafahamishwa kwamba watahakiki pindi watakaporudi nchini kwa kuonesha
vielelezo vya kuthibitisha wa kutokuwepo nchini.
Baada
ya kumaliza awamu ya kwanza ya uhakiki kwa mkoa wa Dar es Salaam, Mamlaka
itaendelea na awamu ya pili katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani. Zoezi litaanza
rasmi tarehe 15/02/2017 na kumalizika tarehe 31/03/2017. Tarehe ya kuanza
kuhakiki katika mikoa mingine iliyobaki itatangazwa baadae.
Pia
kwa watakao bainika kuwa na TIN zaidi ya moja, utaratibu uliopo ni wa kuhuisha
taarifa ya mojawapo ya TIN hizo na kuzifunga nyinginezo. Endapo mtu ana madeni ya kodi katika mojawapo
ya TIN hizo au zaidi, utaratibu wa kudai madeni utaendelea kwa mujibu wa sheria
na Mamlaka haitamzuia mwenye deni kuhakiki TIN yake.
Mamlaka
inatoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano
wa karibu ili kukamilisha zoezi hili kwa wakati. Pia tunawakumbusha wananchi
wote kuwa lengo la zoezi hili ni kuhuisha na kupata taarifa sahihi za mlipakodi
na si vinginevyo.
Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali usisite kuwasiliana na
kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800750075/0800780078
au Barua pepe huduma@tra.go.tz
‘’Pamoja Tunajenga
Taifa Letu’’
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
0 comments:
Post a Comment