Alhaji Ali Hassan Mwinyi akizungumza hii leo na kukasema watanzania wasiwe na hofu juu ya afya yake.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, wakati Mzee Mwinyi alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam jana.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, wakati Mzee Mwinyi alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam jana.
Na Mroki Mroki
Rais Mstaafu wa
awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amezengumza na TSN Digital na kuwatoa
hofu watanzania juu ya afya yake na kusema kuwa yupo vizuri na wala hasumbuliwi
na maradhi yoyote.
Rais Mstaafu
Mwinyi alizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati alipomtembelea na kumjulia
hali Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya, nyumbani kwake Upanga hii leo.
“Ah Mimi niko
vizuri nina afya njema na leo nimefanya mazoezi yangu kama kawaida kwa kutembea
kilometa tano kwa mwendo wa kasi, hivyo niwatoe hofu watanzania na wananchi kwa
ujumla juu ya afya yangu,”alisema Alhaji Mwinyi.
Jana katika
mitandao ya kijamii kulienezwa tarifa kutoka nchini Marekani ambako walisema
Rais huyo alikuwa amelazwa kwa matibabu ya moyo na kufariki Dunia jambo ambalo
si la kweli na kiongozi huyo yupo mwenye afya njema.
Aidha tarifa kutoka
idara ya Habari Maeleozo kupitia Mkurugenzi,
Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas
ilikanisha tarifa hizo na kusema kuwa Mzee Mwinyi ni mzima wa afya, anaendelea
na majukumu yake kama kawaida.
“Jana alihudhuria
chakula cha jioni kuadhimisha siku ya Taifa la Kuwait na leo mchana baada ya
swala ya Ijumaa alimtembelea kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David
Msuya,”ilisema tarifa hiyo.
Dk Abbasi
aliitaka jamii ifahamu kuwa ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya
Makosa ya Mitandaoni, 2015, kwa mtu yeyote kutangaza, kuchapisha au kueneza habari
za uongo au uzushi katika mitandao.
0 comments:
Post a Comment