Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori (kushoto) pamoja na viongozi
wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori akishuhudiwa na
viongozi wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori (kushoto)
akibadilishana mawasiliano na na viongozi wapya wa CCM walioteuliwa
hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo na Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga walipoenda kujitambulisha kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
******************
Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli,
leo tarehe 20 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi watatu
wa CCM aliowateua hivi karibuni kujaza nafasi wazi katika safu ya uongozi wa
chama ngazi ya taifa.
Viongozi hao ni Naibu
Katibu Mkuu Bara Bw. Rodrick Mpogolo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC),
Itikadi na Uenezi Bw. Humphrey Polepole na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC), Siasa na Mambo ya Nje Kanali Mstaafu Ngemela Eslom Lubinga.
Baada ya mazungumzo hayo
yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw.
Humphrey Polepole amesema lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kumweleza
Mwenyekiti wa CCM fikra na mipango ya awali na namna walivyojipanga kwa
kushirikiana na viongozi wengine wa chama, kusimamia na kutekeleza ajenda ya
mageuzi ndani ya chama ambayo msingi wake ni kuirejesha CCM kwa watu.
"Na Mhe. Rais
ametuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba msimamo wa kufanya mageuzi kwenye Chama
Cha Mapinduzi, kukirudisha kwenye misingi ambayo chama hiki kilianzishwa, yaani
chama cha wanyonge na chama ambacho kinajinasibu na shida za watu,
unatekelezwa.
"Ametuambia
tukafanye kazi kwa bidii, Watanzania wana matumaini makubwa sana na Chama Cha
Mapinduzi na sisi tumemhakikisha kwenda kuchapa kazi ili dhamira ya kujenga
Tanzania mpya iweze kuakisiwa na kuletwa na CCM Mpya" amesema Bw.
Polepole.
0 comments:
Post a Comment