Jeshi la Polisi
nchini limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa
wa utapeli anayejulikana kwa jina la Wilfred Masawe (36) , Kabila mchaga
na mkazi wa Buza, Temeke jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa huyo
alikuwa akitumia mbinu mbalimbali kutapeli zikiwemo kujitambulisha kama
kiongozi wa serikali kwa kutumia mtandao wa Whatsapp, huku akieleza kuwa yupo nje ya nchi na kuna
tatizo la msiba ambao umetokea nchini na unamuhusu na hivyo alikua akitoa
maelekezo kwa watendaji wa serikali waweze kusaidia gharama za matibabu
hospitalini, gharama za kusafirisha mwili wa marehemu na gharama za mazishi.
Pia alikuwa
akitumia mbinu ya kujifanya kiongozi mkubwa wa dini ya kikristo (Askofu) na
kuwaambia waumini na viongozi mbalimbali kuhusu maandalizi ya makongamano ya
kidini kwa lengo la kuwaomba michango kuweza kufanikisha makongamano hayo.
Baadhi ya
matukio aliyofanikiwa kutapeli ni pamoja na kuwatapeli viongozi wa serikali,
wafanyabiashara, mameneja na wakurugenzi wa taasisi za umma, wanasiasa pamoja
na waumini wa madhehebu ya dini.
Aidha, matukio
yote hayo alikuwa akiyafanya peke yake na alikua akiyaendesha kwa mawasiliano
ya njia ya ujumbe mfupi (SMS) bila kuzungumza kwa simu.
Jeshi la Polisi
linakamilisha taratibu za kisheria ili mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake.
Jeshi la Polisi nchini linaendelea kutoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa
makini na mtandao wa matapeli hao na yeyote mwenye taarifa za matapeli anaombwa kuzifikisha
haraka katika kituo chochote cha Polisi
kilicho karibu ili waweze kushugulikiwa haraka.
Imetolewa na:-
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
0 comments:
Post a Comment