Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini, Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji akipokea madawati 100 yenye thamani ya Milioni 10 kutoka kwa
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Jema Msuya. Makabidhiano hayo yalifanyika
wilayani Kondoa, Dodoma
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini, Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji akipokea madawati 100 yenye thamani ya Milioni 10 kutoka kwa
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Jema Msuya. Makabidhiano hayo yalifanyika
wilayani Kondoa, Dodoma
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini, Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB,
Jema Msuya baada ya Makabidhiano ya Madawati 100 yenye thamani ya shilingi
milioni 10, Makabidhiano hayo yalifanyika wilayani Kondoa, Dodoma. Wa kwanza
kulia Meneja wa TPB tawi la Dodoma, Twaha Khaflani, wengine ni viongozi wa
Wilaya ya Kondoa.
Msuya alisema misaada inayotolewa na benki hiyo ni sehemu
ya gawio la faida inayopata benki na kuirudishia jamii kwa kuwajengea au
kuunga mkono miradi ya maendeleo. Alisema misaada hiyo inatokana na maombi ya
misaada ya iliyotumwa kwao na Viongozi au Wananchi kwa miradi ya maendeleo
lakini benki imekuwa ikitoa kulingana na bajeti yake inavyoruhusu.
Hata hivyo alisema mpaka sasa benki hiyo imeshatoa madawati zaidi ya
300 mwaka huu na kujenga vyoo na vyumba vya madarasa katika Mikoa mbalimbali
hapa Nchini. Aidha aliongeza kuwa TPB imekuwa ikiunga mkono Serikali kwa
kusaidia Jamii katika sekta ya afya, elimu na ustawi wa jamii.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa fedha na Mipango ambaye pia ni
Mbunge wa jimbo la Kondoa Vijijini, Dkt. Ashatu Kijaji aliishukuru TPB kwa
kutoa msaada huo. Dkt. Kijaji alisema Serikali inatakiwa kuungwa mkono na wadau
wa maendeleo ili kuweza kufanikiwa katika malengo iliyojiwekea ya kuwahudumia
Wananchi. “kwa upendeleo wa kipekee naomba katika madawati haya 100
tuliyopewa madawati 50 yaende shule msingi Kalamba niliyosoma mimi”
aliomba Naibu Waziri.
Naye Afisa Elimu Wilaya Kondoa, Alphonce Mwamwile alisema Wilaya
hiyo ina upungufu wa madawati 5765 yanayohitajika. Aidha aliwaomba wadau
wengine kujitokeza kusaidia changamoto ya madawati na vyumba vya madarasa katika
Wilaya ya hiyo ili Wanafunzi waweze kusoma na kuandika vizuri wakiwa darasani.
0 comments:
Post a Comment