WAZIRI na
Mbunge wa zamani wa jimbo la Mufundi Kaskazini, mkoani Iringa Joseph Mungai amefariki dunia.
Taarifa za kifo cha Mungai zilianza kusambaa leo jioni majira ya saa 12 na baade Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Aminiel Aligaesha kuthibitisha kupokelewa kwa mwili wa kiongozi huyo wa zamani.
Aligaesha alisema Mungai (73) hakuwa
amelazwa Hospitalini hapo ila mwili wake ulipokelewa idara ya magonjwa ya
dharula na kuthibitishwa na madaktari alishafariki saa 11:20 jioni.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
0 comments:
Post a Comment