Rais Dk. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakizindua wamezindua barabara ya
Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika
Jiji la Nairobi nchini Kenya.
Rais Dk. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakizindua wamezindua barabara ya
Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika
Jiji la Nairobi nchini Kenya.
Marais hao wakipata maelezo ya ujenzi wa barabara hiyo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo tarehe 01 Novemba, 2016 wamezindua barabara ya
Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika
Jiji la Nairobi nchini Kenya.
Sherehe ya
uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na inayounganisha maeneo
mbalimbali ya Jiji la Nairobi imefanyika katika eneo la Karen nje kidogo ya
Jiji la Nairobi.
Akizungumza
katika sherehe hiyo Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na Serikali yake
kwa kujenga barabara hiyo ambayo sio tu itawasaidia wananchi wa Kenya bali pia
itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia
Nairobi.
Rais
Magufuli pia ameishukuru Serikali ya China kupitia benki yake ya Exim ambayo
imetoa mkopo wa kujenga barabara hiyo, kwa kuendelea kuziamini nchi za Afrika
Mashariki na kuzikopesha mikopo inayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ikiwemo ujenzi wa barabara.
"Wananchi
wanahitaji maendeleo na haya ndio maendeleo, barabara hii itasaidia kuinua
uchumi na itasaidia masuala ya kijamii" amesema Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli amesema viongozi wa Afrika Mashariki wameamua kufanya kazi ya
kuharakisha maendeleo na kuinua maisha ya wananchi, na kwamba ili kufanikisha
hilo wamedhamiria kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara
zinazounganisha nchi wanachama na kujenga vituo vya pamoja vya utoaji wa huduma
za mpakani (One Stop Border Post).
Kwa upande
wake Rais Kenyatta amesema kujengwa kwa barabara hiyo kumesaidia kupunguza
msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi na pia kutaboresha shughuli za
maendeleo ya wananchi.
Mhe.
Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana nae kuzindua barabara hiyo na
amesema Kenya itaongeza juhudi katika utekelezaji mradi wa ujenzi wa barabara
zinazounganisha Kenya na Tanzania zikiwemo barabara ya Malindi kupitia Saadani
hadi Bagamoyo nchini Tanzania na barabara ya Voi - Taveta- Holili-Arusha.
Sherehe za
uzinduzi wa barabara ya Southern By-pass zimehudhuriwa na Naibu Rais wa Kenya
Mhe. William Ruto.
Kabla ya
kuzindua barabara hiyo Rais Magufuli ametembelea kiwanda kidogo cha kusindika
maziwa cha Eldoville kilichopo katika eneo la Karen ambacho kinamilikiwa na
familia ya mkulima Bw. James Karuga.
Familia hiyo
ilianzisha kiwanda cha kusindika maziwa mwaka 1985 kwa uzalishaji wa chini ya
lita 1,000 kwa siku na hivi sasa imefikia uzalishaji wa lita 5,000 kwa siku na
inatarajia kuongeza uzalishaji hadi lita 70,000 katika mwaka mmoja ujao baada
ya kuongeza kiwanda cha pili.
0 comments:
Post a Comment