Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala akizungumza wa shule ya sekondari Tabora Girls hivi karibuni.
Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na mwalimu wao alipofanya ziara shuleni hapo.
Aidha pamoja na kuzungumza "HAVE FAITH,HOPE FOR MORE AND DREAM EVEN BIGGER", pia aliwaasa kuwa elimu ni msingi mzuri wa maisha na kuwa wasiharakishe na kupotoshwa na mambo ya kidunia kwani haya maisha yapo.
***************
Mrembo
wa taji la Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala amejitosa kusaidia
kurejesha heshima ya mkoa wa Tabora katika elimu hasa kwa wasichana
ambao ndio nguzo kubwa kwa familia na maendeleo ya taifa.
Mrembo
huyo ameamua kufanya hivyo kwa kutembelea shule mbili za Tabora Girls
na Isevya kuongea na wanafunzi, kuwapa moyo na kuangalia matatizo
yanayowasumbua katika kujipatia elimu.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Akizungumza na Moblog
amesema kwamba amekuwa na masikitiko makubwa na matokeo ya mitihani ya
kitaifa ya sekondari kwa miaka mitatu ilhali simulizi za Tabora miaka
iliyopita ni za kufurahisha sana uikionesha kwamba mkoa huo ndio kitovu
hasa cha elimu.
Anasema
ukisoma nyaraka mbalimbali unaona jinsi Tabora ilivyokuwa ngome ya
elimu huku watanzania wengi wakifika hapo pia kupata elimu ya sekondari.
“Kwa
kweli pamoja na masimulizi mazuri kuhusu elimu Tabora miaka ya 80 na 90
,nilichagua Tabora girls kwa sababu ni shule aliyosoma mama yangu mzazi
form 1 mwaka 1977 mpaka 1980 mpaka na aliisifia sana shule yake hiyo na
nikapenda niweze kuwa karibu nao kuhakikisha wanafunzi wote
wanamaliza,na Isevya ilikua chaguo la pili kwasababu ilikua ni shule ya
kutwa (day) na nilipendelea kuongea na wanafunzi hao” alisema Genevieve.
Mkoa
wa Tabora ambao unapatikana kati ya Magharibi ya Tanzania kwenye uwanda
wa latitudo 40-70 Kusini na longitudo 310 - 340 mashariki ukipakana na
mikoa ya Shinyanga, Katavi, Singida, Kigoma na Dodoma ni mji
ulioanzishwa na wafanyabiashara wa Kiarabu kwenye miaka ya 1850
ukijulikana kama Kazeh .
Kihistoria
Kazeh ambayo ilikuwa kitovu cha biashara ya utumwa, mwaka 1871 robo ya
mji ilichomwa moto na kuvurugwa na mtawala wa wanyamwezi Mirambo .
Pamoja na historia yenye misukosuko ya Mkoa wa Tabora ambao ni moja ya mikoa yenye eneo kubwa unategemea sana kilimo kufanikisha maisha lakini kwa miaka mingi mkoa umekuwa ukididimia kimaendeleo na kijamii.
Mkoa
wa Tabora ambao umekua wa mwisho kwa miaka mitatu mfululizo mwaka
2013,2014 na 2015 unahitaji nguvu kubwa ya kujiondoa katika shida ya
kuporomoka katika elimu
Mrembo
Genevieve anasema ziara yake katika shule hizo imemfumbua macho na
kuona haja kubwa ya kuendelea na programu za kufufua matumaini.
Pamoja
na kuwashukuru walimu kwa ushirikiano waliompa aliwataka wanafunzi
kuweka mkazo katika imani, matumaini na kutekeleza ndoto zao katika
uwanda mkubwa zaidi.
Akiwa na wasichana wa shule ya Tabora Girls walimweleza changamoto wanazokutana nazo ikiwa ni pamoja na kutokuwepo na uzio kwenye shule yao hiyo, uhaba wa vitabu, upungufu wa walimu, uhaba wa upatikanaji wa habari mubashara, kwa wanafunzi kwamba hawana king'amuzi,kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wanauhitaji wa msaada wa kofia pamoja na mafuta ya kuwakinga na jua.
Matatizo hayo yanatokana zaidi na kwamba wengi wao wanatoka kwenye mazingira duni. Changamoto nyingine ni pamoja na kuwa na zahanati ambayo ina uhaba wa vifaa mfano:vyandarua vya kutosha pamoja na vitanda,pia kwa wanafunzi ambao wanaulemavu wa macho ambao ni hafifu na vipofu kabisa hivyo kuna uhaba wa brail paper.
Ziara fupi ya Mrembo wa Tanzania 2010 Genevieve Mpangala kwa shule mbili za jijini Tabora za Isevya Secondary School na shule ya vipaji maalum ya wanawake Tabora girls.
Amesema katika mazungumzo yake na wanafunzi hao amebaini pia kwamba kutofanya vyema kwa wanafunzi pia kunasababishwa na wanafunzi hao kutumia madawa ya kulevya, utoro, mimba za shuleni na wazazi kuozesha mabinti katika umri mdogo kabla ya wao kumaliza shule.
0 comments:
Post a Comment