Makamu mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Meru akiwa
anachangia hoja katika baraza hilo
baadhi ya madiwani wa meru wakifuatilia
kikao
Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Christopher
Kazer akifafanua jambo kwa waandishi mara baada ya baraza
kumalizika
mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Christopher
Kazer akijibu hoja mbele ya madiwani wa
meru
baadhi ya madiwani
wakifuatailia
Habari picha na Woinde
Shizza,Arusha
BARAZA la
madiwani Halmashauri ya Meru mkoani Arusha wamkaanga Mkurugenzi
wasema hana uwezo wa kuongoza Halmashauri
hiyo.
Akitoa
maazimio ya kikao cha baraza kilichokaa siku
mbili kilichowajumuisha madiwani,wakuu wa idara mbalimbali na wataalam
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Willy Njau Alisema wametafakari kwa kina
utendaji wa Mkurugenzi na kubaini kuwa hafai.
" Tumejadili ajenda ya utendaji usioridhisha wa
Mkurugenzi
wetu na tumeona kuwa haufai kutokana na mambo mengi anayoyafanya
yanakiuka kanuni na taratibu za Halmashauri"alisema
Njau.
Aidha Njau
alisema Mkurugenzi huyo ameonekana kukata mawasiliano na mwenyekiti wa
Halmashauri jambo alilosema siyo sahihi.
Alisema pia
ameweza kukata mawasiliano na madiwani wa
Halmashauri hiyo pamoja na kusababisha hata wakuu wa idara kutokuwa na
mawasiliano na madiwani jambo linalorudisha maendeleo
nyuma.
Aliongeza
kuwa Mkurugenzi huyo ameshindwa kukusanya
makusanyo ya pesa kiasi cha milioni 150 kilichokusudiwa kukusanywa
tangu Julai hadi septemba mwaka huu jambo alilosema linaweza
kusababisha Halmashauri kutopewa ruzuku kutoka serikali kwasababu ya
uzembe.
"
Tumejiridhisha kuwa uwezo wa Mkurugenzi kuiongoza
Halmashauri yetu kama Mkurugenzi Mtendaji ni mdogo hivyo hafai
anadidimiza maendeleo ya Halmashauri ya meru" alisema Njau. Na
kuongeza.
"Tumeamua
kuiomba mamlaka yake na Uteuzi ichukue hatua stahiki za
kumuwajibisha ili kunusuru maendeleo ya Halmashauri ya
meru"
Vilevile
alisema kuwa Mkurugenzi huyo amekuwa akidharau
maagizo yanayotolewa na kamati mbalimbali za baraza hilo na Kushindwa
kuzitekeleza ambapo ni kuvunja kanuni na taratibu za
Halmashauri.
Hata hivyo
alisema kitendo cha mkurugenzi kukata posho
zamadiwani ni kinyume na utaratibu kwani ziliwekwa kisheria ambapo
alisema Kama kuna tatizo la kukatwa posho ni lazima sheria hiyo
ingebadilishwa kwanza.
" Mwenye
dhamana ya kutangaza kuwa posho zinabadilika ni
Waziri mwenye dhamana hiyo lakini siyo mkuu wa mkoa, Wilaya au
Mkurugenzi" alisema .
Naye Diwani
wa Kikatiti Elisa Mungure ambaye ni Mwenyekiti
wa madiwani alisema Mkurugenzi huyo amekuwa akiendesha Halmashauri
kisiasa jambo ambalo halifai.
"
Ninasikitishwa na uongo unaoelezwa na Mkurugenzi ambaye
kateuliwa na mheshimiwa Rais hii ni ajabu haiwezekani kuendelea
kumuamini mtu wa aina hii" alisema Mungure.
Alisema
Mkurugenzi huyo amekuwa akiwqhamisha watendaji wa
kata bila kufuata taratibu huku akishinikiza ofisi ya kata
ya Kikatiti
kuwa ni ya CCM huku ikiwa ni ofisi ya wananchi wala siyo ya chama
chochote.
Kwa upande
wake mkurugenzi Huyo Christopher Kazer alisema
anafuata maagizo ya mkuu wa nchi na hawezi kuwanyima watu kufikiri
wanavyofikiri.
" Maelekezo
ya kupunguza matumizi yasiyolazima kutoka kwa
mkuu wa nchi ninayafuata pia ndio maana nimepunguza matumizi mengi"
alisema.
Alisema
hawezi kuzuia maamuzi yanayotolewa na baraza hilo
maana kwa namna moja au nyingine wamekaa wakatengeneza maamuzi hivyo
hawezi kuwalazimisha kutofanya maamuzi.
Aidha pia
alibainisha kuwa anaamini kabisa madiwani hawa wanataka halmashauri
iendeshe kisiasa wanataka iendeshwe kama wao wanavyotaka kitu ambacho
hatakubali kwani sio hakutumwa kufanya kazi ya siasa bali alitumwa
kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi na serikali kwa
ujumla
Alisema kuwa
anaamini haya yote yanatokea kutokana na madiwani hawa kukatwa fedha
za posho na usafiri ambao walikuwa wamejiwekea bila kufuata
taratibu
"ivi jamani
ndugu waandishi mtu anatoka apo usa anataka alipwe nauli elfu 80 ni
haki kweli wengine wanatoka apa apa wakija kikao kikichelewa kuisha
wanataka walipwe fedha za kulala laki laki sasa mimi hayo yote
tumeyatoa sasa ivi wanalipwa elfu 40 tu na mshahara wao upo pale pale
sasa wao ndio maana wananipiga zwegwe mimi nasema nitasimamia ilani ya
chama ambacho kinaongoza serikali pia nitafata sera ya muheshimiwa
Rais ya kubana matumizi sitakubali wafanye vitu ovyo na
ninyamaze walifikia atua wakataka hata kunigombanisha na watendaji
wangu ila mimi nimeajiriwa na serikali mimi sio mwanasiasa na
nitafanya kazi kama nilivyoaaidi siku nilioapishwa "alisema
mkurugenzi Kazer
0 comments:
Post a Comment