Hospitali
ya Kairuki katika kuboresha huduma zake kwa wagonjwa imeanza kutumia
kitengo kipya kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kutwa hususani wale
wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Kitengo
hicho kipya (OPD 3) kilichopo nyuma ya Jengo kuu la hospital mkabala
na kitengo cha magonjwa ya viungo (Physiotherapy Unit) kina sehemu kubwa
ya mapokezi, vyumba mbalimbali vikiwemo vyumba 10 via madaktari,
maabara,Duma la dawa,sehemu ya sindano na kufunga vidonda,chumba cha
ultrasound,mapokezi , huduma za chanjo ya watoto (RCH),chumba cha
wauguzi na duka dogo la vinywaji na vitafunwa nk.
Kitengo
hicho kipya kitaiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma kwa haraka na
ufanisi zaidi kwa wagonjwa wasiopungua 120,000 kwa mwaka hivyo kupunguza
kero ya foleni na msongamano iliokuwepo siku za nyuma.
Imetolewa na Afisa
Mahusiano, Arafa Mohamed
0 comments:
Post a Comment