Nafasi Ya Matangazo

October 30, 2016

 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akipokea heshima ya kijeshi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akiwa meza kuu wakiangalia gwaride la Mgambo.

ASKARI wa Jeshi la Mgambo wametakiwa kuacha kushirikiana na wahalifu katika vitendo viovu na kutumia Mafunzo waliyo yapata kuzuia uhalifu na kuzisaidia mamraka za kiraia katika kuimalisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala jana wakati akifunga mafunzo ya Askari Mgambo 65 katika kijiji cha Bukililo kata ya Gwanumbu Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma ambapo aliwaomba Askali hao kutumia mafunzo hayo kwa kutumisha ulinzi katika Vijiji vyao na kushirikiana na Serikali kuwaibua wahalifu.

Ndagala alisema Askali mgambo ni moja kati ya jesi linalo lisaidia Taifa katika ulinzi na usalama na mafunzo mliyo yapata ninaimani yamewajengea uzarendo wa kuipenda Nchi yenu, muyatumie mafunzo haya mlio yapata katika kuhakikisha uhalifu na suala la wahamiaji halamu yana kwisha kabia katika vijiji vyenu.

Alisema vijiji vya Bukililo na Gwanumbu ni vijiji ambavyo vinapakana na Nchi jirani ya Burundi tumeamua kutoa mafunzo haya ilikuongeza askali wa kutosha ilikukomesha vitendo vya kiuhalifu vilivyo kuwa vikiendelea mipakani ikiwa ni pamoja na kuwazuia Wahamiaji halamu ambao wengi wao wanakuja kushirikiana na wahalifu kufanya vitendo vya kiujambazi na kuingiza siraha mbalimbali Nchini.

Aidha Ndagala aliwaomba Wananchi kushirikiana na askari hao kuwafichua wahalifu na wahamiaji halamu ambao baadhi yao wamewapokea na kuwahifadhi bilakujua wanaweza kusababisha madhala gani na wengi wao wameingia na siraha ndio wanao jihusisha na vitendo vya utekaji na kuwaibia wananchi mali zao.

"Niwapongeze kwa kumaliza mafunzo haya ya miezi minne ni mafunzo mazuri na kwamaonyesho mlio yaonyesha ninaimani mtakuwa mabarozi wazuri katika kazi zenu niwaombe msitumie mafunzo hayo kinyume na utaratibu kazi yenu ni kudumisha usalama na kufanya kazi wakati wa vita kama  Askali na kulinda maeneo nyeti msikubali kutumiwa na watu kutimiza malengo yao mtakuwa mkikiuka kiapo mlicho kiapa hii leo",alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Gwanumbu Toi Butono alisema kumalizika kwa mafunzo hayo itasaidia Kijiji kupata Askali wa kutosha awali kijiji kilikuwa hakina askali na matukio ya kiuhalifu yalikuwa yamezidi lakini baada ya kuwapata askali hao vitendo hivyo vitapungua.

Nao Baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo,Efron Reuben na Asuman Manase waliishukuru Serikali kwa kuamua vijana nao wapate mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuimalisha ulinzi na usalama vijijini na kuishi kizalendo katika Nchi yao.

Hata hivyo waliiomba Serikali pindi zinapo tokea nafasi za ulinzi katika taasisi za kiserikali na binafsi wapewe kipaumbele pamoja na nafasi za kujiunga na Jeshi la wanachi (JW) wapewe kipaumbele ilikutoa hamasa kwa vijana na watu wengine kuona umuhimu wa kujiunga na jeshi la mgambo.
Posted by MROKI On Sunday, October 30, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo